10 Wakati tulipokuwa huko kwa siku kadhaa, alifika nabii mmoja aitwaye Agabo kutoka Yudea. 11 Alikuja kutuona akachukua mshipi wa Paulo, akautumia kufunga mikono yake mwenyewe na miguu yake akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwe nye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa mataifa .”’ 12 Tulipo sikia maneno haya sisi na ndugu wengine tulimwomba Paulo asiende Yerusalemu.

Read full chapter