Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini. Na Mungu ambaye anajua mioyo ya watu alishuhudia kwamba anawakubali watu wa mataifa kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa na sisi. Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa sababu waliamini. 10 Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hawa ndugu wanafunzi mzigo wa sheria ambao baba zetu na sisi tumesh indwa kuubeba? 11 Sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Yesu, kama na wao wanavyookolewa.”

Read full chapter