Add parallel Print Page Options

Mmeishi maisha ya anasa duniani na kujifurahisha na kila kitu mlichotaka. Mmeinenepesha miili yenu, kama wanyama walio tayari kwa siku ya kuchinjwa. Mmehukumu na kuua wale watu wasio na hatia, na ambao hawakupingana nanyi.

Uwe Mstahimilivu

Hivyo kina kaka na kina dada, muwe na subira; hadi kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Kumbukeni kuwa mkulima huyasubiria mazao yake yenye thamani yakue ardhini. Huyangoja kwa subira mpaka yapate mvua za masika na za vuli.[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:7 mvua za masika na za vuli “Mvua za masika” zilinyesha mwanzoni na “mvua za vuli” zilinyesha mwishoni.