14 ili kuwafanya Wayahudi wenzangu waone wivu, na hivyo niwaokoe baadhi yao. 15 Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao kumefanya ulimwengu wote upatanishwe na Mungu, kuokolewa kwao je, si kutakuwa ni uhai kutoka kwa wafu? 16 Na kama sehemu ya kwanza ya unga ulioumuliwa ni wakfu, basi unga wote ni wakfu; na kama shina ni wakfu, matawi nayo yatakuwa wakfu.

Read full chapter