Add parallel Print Page Options

Ninamshukuru Mungu kwa namna mlivyonisaidia nilipokuwa ninawahubiri watu Habari Njema. Mlinisaidia tangu siku ya kwanza mlipoamini mpaka sasa. Nina uhakika kwamba Mungu, aliyeianzisha kazi njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka itakapomalizika siku ile ambayo Kristo Yesu atakuja tena.

Ninajua niko sahihi kwa namna ile ninayowawazia ninyi nyote kwa sababu mko karibu sana na moyo wangu. Mmechangia sehemu muhimu sana katika neema ya Mungu kwa ajili yangu wakati huu nikiwa gerezani, na wakati wowote ninapoutetea na kuuthibitisha ukweli wa Habari njema.

Read full chapter