15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo

17 Kwa hiyo nawaambia na kusisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu, ambao wanaon gozwa na mawazo yao yasiyofaa.

Read full chapter