13 Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14 Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa.

Read full chapter