Add parallel Print Page Options

Lakini ni kuhani mkuu tu aliweza kuingia kwenye chumba cha pili, na aliingia mara moja tu kwa mwaka. Pia, asingeweza kuingia ndani ya chumba hicho bila kuchukua damu pamoja naye. Aliitoa damu hiyo kwa Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi walizotenda watu bila kujua kwamba walikuwa wanatenda dhambi.

Roho Mtakatifu hutumia vyumba hivi viwili tofauti kutufundisha kwamba njia ya kuelekea Patakatifu pa Patakatifu haikuwa wazi wakati chumba cha kwanza kilipokuwepo. Huu ni mfano kwetu leo. Inaonyesha sadaka na sadaka ambazo makuhani walizitoa kwa Mungu haziwezi kufanya dhamiri za wanaoabudu ziwe safi kabisa.

Read full chapter