Add parallel Print Page Options

10 Sadaka na sadaka hizi ni kwa ajili tu ya vyakula na vinywaji na aina maalumu ya kuoga. Ni sheria kuhusu mwili tu. Mungu alizitoa kwa watu wake wazifuate hadi wakati wa njia yake mpya.

Ibada Chini ya Patano Jipya

11 Lakini Kristo tayari amekuja awe kuhani mkuu. Yeye ni kuhani mkuu wa mambo mema tuliyonayo sasa. Lakini Kristo hatumiki ndani ya eneo kama hema ambalo makuhani wale walitumika ndani yake. Anatumika katika eneo bora zaidi. Tofauti na hema lile, hili ni kamilifu. Halikutengenezwa hapa duniani. Siyo la ulimwengu huu. 12 Kristo aliingia Patakatifu Zaidi mara moja tu; hii ilitosha kwa nyakati zote. Aliingia Patakatifu Zaidi kwa kutumia damu yake mwenyewe, siyo damu ya mbuzi au ya ng'ombe wadogo. Aliingia hapo na kutuweka huru milele kutoka katika dhambi.

Read full chapter