10 Hizi zilikuwa ni sheria zinazohusu chakula na vinywaji na taratibu mbalimbali za utakaso wa nje, kanuni ambazo zingetumika mpaka wakati wa matayarisho ya utaratibu mpya.

Damu Ya Kristo Husafisha Dhamiri

11 Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12 Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele.

Read full chapter