Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.

Jambo hili linahitaji hekima na maarifa. Vile vichwa saba ni milima saba ambapo huyo mwanamke ameketi. 10 Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao kati yao watano wamekwisha kuanguka, mmoja yupo na mmoja hajaja bado, naye akija, atalazimika kukaa kwa muda mfupi tu.

Read full chapter