Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa damu ya watu wa Mungu na damu ya watu waliouawa kwa kumshuhudia Yesu. Nilipomwona, nilistaajabu sana. Lakini yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufunulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyembeba, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.

Read full chapter