Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakal dayo akaenda kukaa Harani. Baba yake alipokufa, Mungu akamtoa huko akamweka katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. Lakini Mungu hakumpa urithi wo wote katika nchi hii, hakumpa hata mita moja ya ardhi. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto. Mungu alimwambia maneno haya, ‘Wazao wako wataishi ugenini, ambapo watafanywa kuwa watumwa na kutendewa maovu kwa kipindi cha miaka mia nne.

Read full chapter