Paulo Afikishwa Mbele Ya Mfalme Agripa

13 Baada ya siku chache mfalme Agripa na Benike wakafika Kaisaria kumkaribisha Festo. 14 Kwa kuwa walikuwa wanakaa Kais aria kwa muda mrefu, Festo alipata nafasi ya kujadiliana na mfalme kesi ya Paulo; akamwambia, “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Feliksi alimwacha gerezani kama mfungwa. 15 Nilipokwenda Yerus alemu, makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka yao juu yake wakitaka ahukumiwe.

Read full chapter