Add parallel Print Page Options

Hivyo Ibrahimu akaondoka katika nchi ya Ukaldayo[a] na kwenda kuishi Harani. Baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta katika nchi hii, mahali mnapoishi sasa. Lakini Mungu hakumpa Ibrahimu sehemu yoyote ya ardhi hii, hata eneo dogo lenye ukubwa wa unyayo wake. Lakini Mungu aliahidi kuwa atampa Ibrahimu nchi hii yeye na watoto wake hapo baadaye. Hii ilikuwa kabla Ibrahimu hajapata watoto.

Mungu alimwambia: ‘Wazao wako wataishi katika nchi nyingine. Watakuwa wageni. Watu wa huku watawafanya kuwa watumwa na kuwatendea vibaya kwa miaka mia nne.

Read full chapter

Footnotes

  1. 7:4 Ukaldayo Au “Babeli”, nchi iliyo kusini mwa Mesopotamia. Tazama mstari wa 2.