Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa?

Read full chapter