31 Kwa hiyo nawaambieni, watu watasamehewa kila aina ya dhambi na kufuru lakini mtu ata kayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

32 “Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.”

Maneno Huonyesha Hali Ya Moyo

33 “Ili upate matunda mazuri lazima uwe na mti mzuri; ukiwa na mti mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake.

Read full chapter