27 Na kama mimi hutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao ndio watakaowaamulia. 28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.

Read full chapter