16 Lakini wakati wo wote mtu anapomgeukia Bwana, “kitambaa kinaondolewa.” 17 Basi, Bwana ni Roho, na mahali alipo Roho wa Bwana pana uhuru. 18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye, kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana ambaye ni Roho.

Read full chapter