15 Hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama ndugu yetu mpendwa Paulo alivyokwisha kuwaandikieni kwa hekima aliyopewa na Mungu. 16 Ameandika hivyo hivyo katika barua zake zote akizun gumzia mambo haya. Barua zake zina mambo mengine ambayo ni magumu kuelewa, ambayo watu wajinga na wasio na msimamo huyapotosha, kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko; na hivyo wana jiletea kuangamia.

Read full chapter

15 Kumbukeni kuwa tumeokolewa kwa sababu Bwana wetu ni mvumilivu. Ndugu yetu mpendwa Paulo aliwaambia jambo hili hili alipowaandikia kwa hekima aliyopewa na Mungu. 16 Ndivyo anavyosema katika barua zake zote anapoandika kuhusu mambo haya. Sehemu zingine katika barua zake ni ngumu kuzielewa, na kuna baadhi ya watu huzifafanua vibaya. Watu hawa ni wajinga na wasioaminika. Watu hawa hutoa pia maana potofu kwa Maandiko mengine. Lakini kwa kufanya hivi wanajiangamiza wao wenyewe.

Read full chapter