Hata kama barua yangu iliwasikitisha, sasa sijuti kwamba niliiandika ingawa nilikuwa nimejuta. Naona barua yangu iliwahu zunisha, lakini kwa muda mfupi. Lakini sasa ninafurahi, si kwa kuwa mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunika kama Mungu anavyopenda watu wahuzunike na hivyo hatukuwadhuru kwa njia yo yote.

Read full chapter

Hata kama barua nilyowaandikieni iliwahuzunisha, sijutii kuiandika. Nafahamu kuwa barua ile iliwatia huzuni, ninasikitika kwa hilo. Lakini iliwapa huzuni kwa muda mfupi. Sasa ninafurahi, si kwa sababu mlipata huzuni, bali kwa sababu huzuni yenu iliwasababisha mkaamua kubadilika. Hilo ndilo ambalo Mungu alilitaka, hivyo hatukuwaumiza kwa namna yo yote.

Read full chapter