Na hata kama Injili yetu imefichika, basi imefichika kwa wale wanaopotea. Kwa upande wao, mungu wa dunia hii ametia giza akili za wasioamini, ili wasione mwanga wa Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ana sura ya Mungu. Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung’aao katika uso wa Kristo.

Read full chapter

Habari Njema tunazowahubiri watu hazijafichika kwa yeyote isipokuwa kwa waliopotea. Mtawala[a] wa dunia hii amezitia giza akili za wasioamini. Hawawezi kuona nuru ya Habari Njema; ujumbe juu ya uungu wa Kristo, taswira halisi ya Mungu. Hatuwaambii watu habari zetu wenyewe. Lakini tunawaambia habari za Kristo Yesu kuwa ni Bwana, na tunawaambia kuwa sisi ni watumwa wenu kwa ajili ya Yesu. Kuna wakati Mungu alisema, “Na nuru ing'ae gizani”[b] na huyu ni Mungu yule yule anayesababisha nuru ing'ae katika mioyo yetu ili tutambue utukufu wa uungu wake mkuu unaongaa katika sura ya Kristo.

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:4 Mtawala Kwa maana ya kawaida, “Mungu”. Lakini usemi huu hapa unamaanisha “Shetani”.
  2. 4:6 Tazama Mwa 1:3.