Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho iliyoan dikwa katika mioyo yenu, ijulikane na kusomwa na kila mtu. Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai.

Read full chapter

Hapana, ninyi wenyewe ni barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu. Inafahamika na kusomwa na watu wote. Mnaonyesha kuwa ninyi ni barua toka kwa Kristo aliyoituma kupitia sisi. Barua ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa katika mbao za mawe[a] lakini katika mioyo ya wanadamu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:3 mbao za mawe Ina maana ya sheria ambayo Mungu aliitoa kwa Musa, iliyoandikwa kwenye mbao za mawe. Pia katika mstari wa 7. Tazama Kut 24:12; 25:16.