Maono Ya Paulo Na Mwiba Aliokuwa Nao

12 Inanibidi nijisifu. Ingawa hakuna faida, nitawaeleza juu ya maono na mafunuo niliyopata kutoka kwa Bwana. Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka.

Read full chapter

Nguvu ya Paulo Inatoka Katika Udhaifu

12 Inanipasa kuendelea kujivuna juu yangu mwenyewe. Hiyo haitasaidia, lakini nitazungumza juu ya maono na mafunuo kutoka kwa Bwana. Ninamjua mtu mmoja[a] katika Kristo aliyechukuliwa juu katika mbingu ya tatu. Hili lilitokea miaka 14 iliyopita. Sifahamu ikiwa mtu huyu alikuwa ndani ya mwili wake au nje ya mwili wake, lakini Mungu anajua. 3-4 Na ninajua kuwa mtu huyu alichukuliwa juu paradiso. Sijui kama alikuwa katika mwili wake au nje ya mwili wake. Mungu pekee ndiye anajua. Lakini mtu huyu aliyasikia mambo ambayo hana uwezo wa kuyasimulia. Alisikia mambo ambayo mtu yeyote anaruhusiwa kuyasema. Read full chapter

Footnotes

  1. 12:2 mtu mmoja Katika sura 12:2-5 Paulo huenda anasema habari zake mwenyewe.