Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda; kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani. Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanayoyasema ni ya ulimwengu na watu wa dunia huwasikiliza. Sisi ni wa Mungu. Anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiye wa Mungu hatusikilizi. Na hivi ndivyo tunaweza kutambua kati ya Roho wa kweli na roho wa uongo.

Mungu Ni Upendo

Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

Read full chapter