Neno La Uzima

Tunawaandikieni kuhusu kile ambacho kimekuwapo tangu mwanzo, ambacho tumekisikia na kukiona kwa macho yetu; ambacho tumekigusa kwa mikono yetu; yaani Neno la uzima. Uzima huo uli tokea, nasi tumeuona na tunaushuhudia, na tunawatangazieni uzima wa milele uliokuwa kwa Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. Tunawa tangazia hicho tulichokiona na kukisikia ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi. Na ushirika tulio nao ni wetu na Baba na Mwa nae Yesu Kristo. Tunawaandikieni mambo haya ili furaha yetu ikamilike.

Kutembea Nuruni

Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia: Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe. Tukisema tuna ushirika naye huku tunaendelea kuishi gizani tunasema uongo, wala hatutendi yaliyo ya kweli. Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote.

Read full chapter