Kufufuka Kwa Wafu

12 Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, inakuwaje baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13 Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi Kristo hakufufuliwa. 14 Na ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, mahubiri yetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Na zaidi ya hayo, tunaonekana kuwa tunamshuhudia Mungu uongo, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu ya kuwa alimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Na kumbe hakumfu fua, kama kweli wafu hawafufuliwi. 16 Kwa kuwa kama wafu hawa fufuliwi, basi hata Kristo hajafufuliwa. 17 Na ikiwa Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni bure; nanyi bado mngali katika dhambi zenu. 18 Pia waamini wote waliokufa wakimwamini Yesu wamepotea. 19 Na kama imani yetu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, basi sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wengine wo wote duniani. 20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wote waliolala.

Read full chapter