Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, sitawasifu!

23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale maagizo niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru , akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywa katika kikombe hiki, mnatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja.

27 Kwa hiyo mtu ye yote anayekula mkate huo au kukinywea kikombe hicho isivyostahili, atakuwa na hatia juu ya mwili na damu ya Bwana. 28 Kila mtu ajichunguze mwenyewe, na ndipo aule mkate na kukinywea kikombe. 29 Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30 Na hii ndio sababu wengi wenu ni wagonjwa na dhaifu, na wengine wamekufa. 31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingalihukumiwa. 32 Tunapohukumiwa na Bwana, anaturudi ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana pamoja kula, ngojaneni. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani ili mnapokutana pamoja msije mkahukumiwa. Na nitakapokuja nitawapa maagizo zaidi.

Read full chapter