15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni sifa kwake. Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu za kumfunika. 16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.

Chakula Cha Bwana

17 Kuhusu maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu kwa sababu mikutano yenu inaleta madhara zaidi kuliko mema. 18 Kwanza, mna pokutana kama kanisa nasikia kwamba kuna mgawanyiko kati yenu, na kwa kiasi fulani naamini ndivyo ilivyo. 19 Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili wale walio wa kweli waweze kuonekana.

20 Mnapokutana pamoja hamli chakula cha Bwana. 21 Kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anaendelea na chakula chake bila kun goja wengine, na mmoja anabaki na njaa wakati mwingine analewa. 22 Je, hamwezi mkala na kunywa kwenye nyumba zenu? Au mnadharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na kitu? Niwaambie nini?

Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, sitawasifu!

23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale maagizo niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru , akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywa katika kikombe hiki, mnatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja.

27 Kwa hiyo mtu ye yote anayekula mkate huo au kukinywea kikombe hicho isivyostahili, atakuwa na hatia juu ya mwili na damu ya Bwana. 28 Kila mtu ajichunguze mwenyewe, na ndipo aule mkate na kukinywea kikombe. 29 Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30 Na hii ndio sababu wengi wenu ni wagonjwa na dhaifu, na wengine wamekufa. 31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingalihukumiwa. 32 Tunapohukumiwa na Bwana, anaturudi ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana pamoja kula, ngojaneni. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani ili mnapokutana pamoja msije mkahukumiwa. Na nitakapokuja nitawapa maagizo zaidi.

Read full chapter