Add parallel Print Page Options

Kondoo wa Mungu

Sasa nina jambo la kuwaambia wazee walio katika kundi lenu. Mimi pia ni mzee nami mwenyewe nimeyaona mateso ya Kristo. Na nitashiriki katika utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Hivyo ninawasihi, mlitunze kundi la watu mnalowajibika kwalo. Ni kundi lake Mungu.[a] Basi lichungeni kwa moyo wa kupenda na si kwa kulazimishwa. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka. Fanyeni hivyo kwa sababu mnafurahi kutumika, na si kwa sababu mnataka pesa. Msiwaongoze wale mnaowasimamia kwa kuwaamrisha. Lakini muwe mfano mzuri wa kuiga kwao.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:2 kundi lake Mungu Watu wa Mungu. Ni kama kundi la kondoo linalotakiwa kutunzwa.