Ondoeni chachu ya zamani ili mpate kuwa donge lisilo na chachu, kama mnavyotakiwa kuwa. Kwa maana Kristo ambaye ndiye Mwana-kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kama dhabihu. Kwa hiyo, tusherehekee sikukuu hii, sio kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu bali kwa mkate usiotiwa hamira, wa moyo safi na kweli.

Read full chapter

Ondoeni chachu ya zamani ili muwe donge jipya. Ninyi kwa hakika ni mkate usio na chachu, mkate wa Pasaka,[a] Ndiyo, Kristo aliye Mwanakondoo wetu wa Pasaka[b] amekwisha usawa. Hivyo na tuule mlo wetu wa Pasaka, lakini si pamoja na mkate wenye chachu ya zamani, yaani dhambi na matendo mabaya. Lakini tule mkate usio na chachu. Huu ni mkate wenye ukweli na chachu njema.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:7 mkate wa Pasaka Mkate maalum usio na chachu (chachu) ambao Wayahudi walikula katika mlo wa Pasaka. Paulo anamaanisha kuwa waamini hawana dhambi, kama ambavyo mkate wa Pasaka haukuwa na chachu.
  2. 5:7 Mwanakondoo wetu wa Pasaka Yesu alikuwa sadaka kwa ajili ya watu wake, kama mwanakondoo aliyechinjwa kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi.