Chakula Kilichotolewa Sadaka Kwa Sanamu

Sasa kuhusu chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Tuna jua kwamba ‘sisi sote tuna ujuzi.’ Lakini ‘ujuzi’ huleta maji vuno, ila upendo hujenga. Mtu anayedhania kwamba anajua kitu, basi hajafahamu kama inavyompasa kujua. Lakini kama mtu anam penda Mungu, mtu huyo anajulikana na Mungu.

Kwa hiyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua kwamba ‘sanamu haina uhai wa kweli’ na kwamba ‘kuna Mungu mmoja tu.’ Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa ‘miungu,’ kama ni mbinguni au duniani; na kwa kweli wapo ‘miungu’ wengi na ‘mabwana’ wengi; sisi tunajua kwamba kuna Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka kwake, na sisi tunaishi kwa ajili yake; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye vitu vyote vimekuwepo kupitia kwake na tunaishi kutokana naye.

Lakini si wote wanajua mambo haya. Watu wengine mpaka leo bado wamezoea miungu ya sanamu kiasi ambacho wanapokula chakula hicho wanadhani ni chakula kilichotolewa kwa sanamu, na kwa kuwa dhamiri yao ni dhaifu, inadhurika. Lakini chakula hakitusaidii kuwa karibu zaidi na Mungu. Hatupotezi cho chote tusipokula, wala hatupati faida yo yote kama tukila.

Lakini hata hivyo tuwe waangalifu jinsi tunavyotumia uhuru wetu tusije tukawakwaza walio dhaifu katika imani. 10 Kwa maana kama mtu mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi mkila katika hekalu la sanamu, je, si atavutwa kula chakula kilichoto lewa kwa sanamu? 11 Kwa njia hiyo, huyo ndugu mwenye dhamiri dhaifu, ambaye Kristo alimfia, atateketea kwa sababu ya ujuzi wako. 12 Mnapowatenda dhambi ndugu zenu kwa njia hii na kuharibu dhamiri zao dhaifu, mnamkosea Kristo. 13 Kwa hiyo kama chakula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.

Kuhusu Vyakula Vinavyotolewa kwa Sanamu

Sasa nitaandika kuhusu suala jingine mliloniandikia mkiuliza kuhusu nyama iliyotolewa sadaka[a] kwa sanamu. Ni kweli kuwa “Sote tuna ujuzi”, kama mnavyosema. Lakini ujuzi huu unawajaza watu majivuno. Upendo ndiyo unaolisaidia kanisa kuwa imara. Wale wanaodhani kuwa wanajua jambo fulani bado hawajui chochote kwa namna inavyopaswa. Lakini Mungu anamjua mtu anayempenda.

Hivyo sasa vipi kuhusu kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu? Tunajua kuwa “sanamu si lolote katika ulimwengu” huu na tunajua kuwa “kuna Mungu mmoja tu”. Baadhi ya watu husema kuwa kuna miungu wanaoishi mbinguni na miungu wengine huishi duniani. Hata kama kuna “miungu” na “mabwana” wanaoaminiwa na watu, hilo si muhimu kwetu. Tuna Mungu mmoja tu, na ambaye ndiye Baba yetu. Vitu vyote vilitoka kwake nasi tunaishi kwa ajili yake. Na kuna Bwana mmoja tu, Yesu Kristo. Vitu vyote viliumbwa kupitia yeye, nasi tunaishi kwa ajili yake.

Lakini si watu wote wanaojua hili. Baadhi ya watu walikuwa na tabia ya kuabudu sanamu huko nyuma. Hivyo wanapokula nyama, bado wanahisi kuhukumiwa kana kwamba wanakula nyama iliyotolewa kwa sanamu. Hawana uhakika ikiwa ni sahihi kula nyama. Lakini chakula hakitatuweka karibu na Mungu. Kukataa kula hakutufanyi tumpendeze kidogo Mungu wala kula hakutuweki karibu na Mungu.

Lakini iweni makini na uhuru wenu. Uhuru wa kula kitu unaweza kuwafanya walio na mashaka wakaanguka katika dhambi kwa kula vyakula hivyo. 10 Mnaelewa kuwa inaruhusiwa kula kitu chochote, hivyo unaweza kula hata katika hekalu la sanamu. Lakini hilo linaweza kumfanya mtu mwenye mashaka akaona kuwa kula chakula kama hicho ni kitendo cha kuabudu sanamu. 11 Hivyo ndugu huyu aliye dhaifu, ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, anaweza akaangamizwa kwa sababu ya uelewa wako ulio mzuri zaidi. 12 Unapomtenda dhambi kinyume cha ndugu zako walio katika Kristo kwa namna hii na unawaumiza kwa kuwafanya wafanye mambo wanayoyachukulia kuwa mabaya, nawe pia unamtenda dhambi Kristo. 13 Hivyo ikiwa chakula ninachokula kinamfanya mwamini mwingine kutenda dhambi, siwezi kula chakula hicho tena. Nitaacha kula chakula hicho ili nisimfanye ndugu yangu atende dhambi.

Footnotes

  1. 8:1 sadaka Mnyama aliyechinjwa na kutolewa kuonesha ibada. Pia katika mstari wa 10.