Font Size
Marko 1:1-6
Neno: Bibilia Takatifu
Marko 1:1-6
Neno: Bibilia Takatifu
Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji
1 Huu ni mwanzo wa Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Kama alivyoandika nabii Isaya, Mungu alisema: “Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye ataandaa njia yako.” 3 “Mtu aitaye kwa sauti kuu jangwani. ‘Mtengenezeeni Bwana njia; nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”
4 Yohana alitokea nyikani, akawabatiza watu huko na kuwahubi ria kwamba watubu, wabatizwe, ili wasamehewe dhambi zao. 5 Watu kutoka eneo lote la Yudea na sehemu zote za Yerusalemu walikwenda kumsikiliza. Wakatubu dhambi zao, akawabatiza katika mto wa Yor dani. 6 Yohana alivaa mavazi ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa ni nzige na asali ya mwituni.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica