A A A A A
Bible Book List

Matendo Ya Mitume 18:23-22:30 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

23 Alikaa Antiokia kwa muda, na baadaye aliondoka akatembelea makanisa huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha waamini wote.

Apolo Ahubiri Efeso Na Korintho

24 Basi Myahudi mmoja jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksan dria alikuja Efeso. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhu biri na pia aliyajua Maandiko barabara. 25 Alikuwa amefundishwa njia ya Bwana naye akiwa amejaa moto wa kiroho alifundisha kwa usahihi juu ya Yesu. Lakini ujuzi wake uliishia kwenye ubatizo wa Yohana. 26 Apolo alihubiri kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27 Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28 maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.

Waamini Wa Efeso Wapokea Roho Mtakatifu

19 Wakati Apolo alikuwa Korintho, Paulo alipitia sehemu za kaskazini akafika Efeso. Huko aliwakuta wanafunzi kadhaa, aka wauliza, “Mlipoamini mlipokea Roho Mtakatifu?” Wakajibu, “Hapana. Hatujawahi hata kusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” Ndipo Paulo akawauliza, “Mlibatizwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Ubatizo wa Yohana.” Paulo akasema, “Yohana alipobatiza, aliwaambia watu watubu dhambi na kumwamini atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Yesu. Na Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia , wakasema kwa lugha mpya na kutabiri. Walikuwepo kama watu kumi na wawili.

Paulo akaingia katika sinagogi na kwa muda wa miezi mitatu akafundisha kwa ujasiri akitumia kila njia kueleza juu ya Ufalme wa Mungu. Lakini baadhi yao walipokataa kuamini na kuanza kukashifu ujumbe wake mbele ya ushirika wote, aliachana nao, akawachukua wale wanafunzi akaendelea kujadiliana nao katika ukumbi wa Tirano. 10 Aliendelea na kazi hii kwa muda wa miaka miwili mpaka wenyeji wote wa Asia wakawa wamesikia neno la Bwana,

Wana Wa Skeva Wajaribu Kutoa Pepo

11 Na Mungu alifanya miujiza mingi ya ajabu kwa mkono wa Paulo. 12 Watu wakachukua vitambaa na taulo ambazo zilikuwa zimegusa mwili wa Paulo wakawawekea wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao na pepo wachafu wakawatoka. 13 Baadhi ya Wayahudi waliokuwa wakienda huku na huko wakiwatoa watu pepo wachafu wali jaribu nao kutumia jina la Yesu kutoa pepo, wakisema, “Nakuamuru kwa jina la Yesu, anayehubiriwa na Paulo.” 14 Palikuwa na wana saba wa kuhani mkuu aliyeitwa Skeva ambao walikuwa wakifanya hivi. 15 Lakini pepo mchafu akawajibu, “Yesu namfahamu na Paulo pia namfahamu; lakini ninyi ni nani?” 16 Yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia akawashambulia vikali, wakatoka ndani ya ile nyumba mbio wakiwa uchi na wenye majeraha. 17 Jambo hili likajulikana kwa wenyeji wote wa Efeso, Wayahudi kwa Wagiriki; hofu ikawajaa watu wote; na jina la Bwana likaheshimiwa. 18 Waamini wengi wakatubu matendo yao maovu hadharani. 19 Na wale waliokuwa wakishiriki uchawi na kupiga ramli wakaleta vitabu vyao na kuvichoma moto hadharani. Walipopiga hesabu ya vitabu walivyochoma walikuta kwamba thamani yake ilikuwa vipande elfu hamsini vya fedha. 20 Neno la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.

Ghasia Huko Efeso

21 Baada ya mambo haya kutokea, Paulo aliongozwa na Roho kupitia Makedonia na Akaya akiwa njiani kwenda Yerusalemu. Paulo alisema, “Nikishafika Yerusalemu, ni lazima niende Rumi pia.” 22 Akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, naye akakaa Asia kwa muda kidogo zaidi. 23 Wakati huo huo pakatokea ghasia kubwa kwa sababu ya Njia ya Bwana. 24 Mtu mmoja aitwaye Demetrio mhunzi wa vinyago vya fedha alikuwa akitengeneza vihekalu vya fedha vya Artemi na kuwa patia mafundi wake biashara kubwa. 25 Yeye aliwakutanisha watu hawa pamoja na watu wengine wanaofanya kazi za kutengeneza viny ago vya miungu kama wao akawaambia, “Jamani, mnajua ya kuwa uta jiri wetu unatokana na kazi zetu. 26 Lakini mmeona na kusikia jinsi ambavyo huko Efeso na karibu Asia yote huyu Paulo amewash awishi watu na kutuharibia biashara kwa kusema kuwa miungu iliy otengenezwa na watu si miungu ya kweli. 27 Kwa hiyo kuna hatari kuwa kazi yetu itaanza kudharauliwa. Na si hivyo tu, bali hata hekalu la mungu wetu Artemi, aliye mkuu na anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa halina maana tena na utukufu wake utaondolewa.”

28 Waliposikia maneno haya walighadhabika wakapiga kelele, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 29 Mji mzima ukajaa vurugu, waka kimbilia katika ukumbi wa michezo kwa pamoja wakawakamata Gayo na Aristarko, Wamakedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo. 30 Paulo alitaka kuingilia kati lakini wanafunzi wengine wakam zuia; 31 hata baadhi ya viongozi waliokuwa marafiki wa Paulo walituma watu wamsihi asiingie katika ule ukumbi. 32 Pakawa na kutokuelewana katika ule ukumbi kwa sababu baadhi ya watu wali kuwa wakisema jambo moja na wengine lingine. Ikawa ni fujo; wengi wa watu waliofika hawakujua ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko. 33 Wayahudi wakamchagua Aleksanda azungumze kwa niaba yao naye akawaashiria watu wanyamaze apate kuzungumza. 34 Lakini umati ulipogundua yakuwa yeye ni Myahudi, walipiga kelele kwa kiasi cha saa mbili wakisema, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 35 Baadaye karani wa mji alipofanikiwa kuwanyamazisha, aliwahu tubia akasema, “Ndugu Waefeso, kila mtu ulimwenguni anajua ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu iliyoanguka kutoka angani. 36 Kwa hiyo, kwa kuwa hakuna anayeweza kukanusha mambo haya, sioni sababu ya ninyi kufanya fujo au kuchukua hatua ambazo baadaye huenda mkazijutia. 37 Kwa maana mmewaleta hawa watu wawili hapa ingawa wao hawaja fanya uharibifu wo wote kwa hekalu la Artemi au kusema maneno ya kufuru juu ya huyu mungu wetu mwanamke. 38 Kama Demetrio na mafundi wenzake wana mashtaka juu ya mtu ye yote, mahakama ziko wazi na mahakimu wapo; wachukue hatua za kisheria. 39 Lakini kama kuna mashauri mengine, itabidi mtumie baraza halali. 40 Hivi sasa tuko katika hatari ya kushtakiwa kwa kufanya fujo kwa maana hatuna sababu ya kuridhisha kuhusu mambo yaliyotokea leo.” 41 Baada ya kusema haya akavunja mkutano.

Paulo Aenda Makedonia na Ugiriki

20 Fujo zilipokwisha, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawa tia moyo halafu akawaaga. Akaanza safari yake ya kwenda Makedo nia. Alipokuwa akisafiri, aliwapa waamini katika sehemu zote alizopita maneno ya kuwatia moyo, ndipo akaenda Ugiriki ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa akijiandaa kwenda Siria kwa meli, iligundulika kwamba Wayahudi walikuwa na mpango wa kumwua, kwa hiyo akaamua kurudi akipitia Makedonia. Watu waliofuatana naye safarini ni Sopatro Piro mwenyeji wa Beroya , Aristako na Sekundo kutoka Thesalonike, Gayo mwenyeji wa Derbe; Timotheo, Tikiko na Trofimo wenyeji wa Asia. Hawa walitutangu lia wakaenda kutungojea Troa. Sisi tuliondoka baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa hamira tukasafiri kwa meli na kuungana nao siku tano baadaye huko Troa ambako tulikaa kwa siku saba.

Paulo Akutana Na Waamini Wa Troa

Jioni siku ya kwanza ya Juma tulikuwa tumekutana pamoja kwa chakula na Paulo akaongea nao akiwa na mpango wa kuondoka kesho yake; akaendelea na mazungumzo mpaka usiku wa manane. Chumba cha ghorofani walipokuwa wakikutania kilikuwa na taa nyingi na kijana mmoja jina lake Eutiko alikuwa amekaa dirishani. Paulo alivyoendelea kuongea kijana huyu alizidi kusinzia. Hatimaye alishikwa na usingizi kabisa, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu, akadhaniwa kuwa amekufa. 10 Lakini Paulo alishuka chini akainama, akamkumbatia yule kijana akasema, “Msiwe na hofu, yun gali hai.” 11 Paulo akarudi ghorofani na alipokwisha kula, akaongea nao tena mpaka alfajiri ndipo akaondoka. 12 Yule kijana alichukuliwa nyumbani akiwa hai na wote waliokuwepo walifarijika.

Paulo Atoka Troa Kwenda Mileto

13 Tuliingia katika meli tukasafiri mpaka Aso ambako tuli tarajia kumchukua Paulo kwa maana alikuwa amepanga kusafiri nchi kavu mpaka huko. 14 Alipotukuta huko Aso, tulimchukua melini tukasafiri wote mpaka Mitilene. 15 Kutoka Mitilene tuliendelea kwa meli na kesho yake tukafika pwani ya upande wa pili wa Kio. Siku iliyofuata tukafika Samo na kesho yake tukawasili Mileto. 16 Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi katika jimbo la Asia; kwa sababu alitaka kama ikiwezekana afike Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.

Paulo Anawaaga Wazee Wa Kanisa La Efeso

17 Paulo akiwa Mileto, alituma ujumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa wakutane naye. 18 Walipofika aliwaambia, “Ninyi mnajua jinsi nilivyoishi nanyi tangu siku ya kwanza nilipofika Asia. 19 Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu na machozi na kwa mateso yaliyotokana na njama za Wayahudi. 20 Mnajua jinsi ambavyo sikusita kuwaambia cho chote ambacho kingekuwa cha faida kwenu, na jinsi nilivyofundisha hadharani na nyumba kwa nyumba 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki juu ya kutubu dhambi kwa Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Na sasa nimevutwa na Roho niende Yerusalemu na sijui mambo yatakayonipata huko. 23 Ila katika kila mji niliopitia, Roho Mtakatifu amenifunulia kwamba mbele yangu kifungo na mateso vinaningoja. 24 Lakini nay ahesabu maisha yangu kuwa si kitu cha thamani kwangu, ili mradi niweze kukamilisha wito na kazi niliyopewa na Bwana Yesu; kazi ya kuwashuhudia watu kuhusu Habari Njema ya neema ya Mungu. 25 Na sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja wenu, ninyi ambao kati yenu nimekuwa nikihubiri juu ya Ufalme wa Mungu, atakayeniona tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wazi leo hii kwamba sina lawama juu ya mtu ye yote kati yenu, 27 kwa sababu sikuacha kuwatangazia mpango kamili wa Mungu. 28 Jilindeni nafsi zenu, na mlinde kundi lote la kondoo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka chini ya uongozi wenu; mtunze kanisa la Mungu ambalo amelinunua kwa damu ya Mwa nae. 29 Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. 30 Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate. 31 Kwa hiyo muwe macho; mkumbuke jinsi nilivyomwonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu. 32 Na sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake ambalo linaweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi pamoja na wote ambao wameta kaswa. 33 Sikutamani fedha au dhahabu au nguo za mtu ye yote. 34 Ninyi wenyewe mnajua kwamba kwa mikono yangu nimefanya kazi nikapata mahitaji yangu na ya wenzangu. 35 Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii mtaweza kuwa saidia walio dhaifu, mkikumbuka maneno aliyosema Bwana Yesu kwamba, ‘Kuna baraka kubwa zaidi katika kutoa kuliko kupokea.”’

36 Paulo alipomaliza kusema haya alipiga magoti akaomba pamoja nao wote. 37 Na wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kum busu, 38 wakihuzunika kwa sababu ya maneno aliyowaambia kwamba hawatamwona tena. Wakamsindikiza wakamfikisha kwenye meli.

Paulo Aenda Yerusalemu

21 Tulipokwisha agana nao tuliondoka tukasafiri moja kwa moja, mpaka Kosi, na siku ya pili yake tukafika Rodo, na kutoka huko tukaenda Patara. Hapo tukapata meli iliyokuwa ikielekea Foinike tukaingia ndani tukasafiri nayo. Tulipokaribia kisiwa cha Kipro, tulikizunguka upande wa kushoto, tukasafiri mpaka Siria, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ili kuwa ipakue shehena yake. Tukawatafuta waamini wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale waamini wakiwa wameongozwa na Roho walim wambia Paulo asiende Yerusalemu. Muda wa kukaa nao ulipokwisha, tuliendelea na safari yetu na wale ndugu waamini pamoja na wake zao na watoto wao walitusindikiza hadi nje ya mji. Wote tulipiga magoti pale pwani tukaomba, kisha tukaagana.

Ndipo tukaingia ndani ya meli na wale ndugu wakarudi mak wao. Tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu waamini wa huko na tukakaa nao kwa siku moja. Kesho yake tuliondoka tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo ambaye alikuwa kati ya wale watu saba waliochaguliwa kule Yerusalemu, tukakaa kwake. Filipo alikuwa na binti wanne ambao walikuwa bado hawajaolewa nao walikuwa na karama ya unabii. 10 Wakati tulipokuwa huko kwa siku kadhaa, alifika nabii mmoja aitwaye Agabo kutoka Yudea. 11 Alikuja kutuona akachukua mshipi wa Paulo, akautumia kufunga mikono yake mwenyewe na miguu yake akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwe nye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa mataifa .”’ 12 Tulipo sikia maneno haya sisi na ndugu wengine tulimwomba Paulo asiende Yerusalemu. 13 Lakini Paulo alijibu, “Kwa nini mnanivunja moyo kwa machozi yenu? Mimi niko tayari kufungwa na hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.” 14 Na kwa kuwa hatukuweza kumshawishi asiende, tuliacha kumsihi tukamwambia, “Mapenzi ya Bwana na yatendeke.”

15 Baadaye tulijiandaa tukaondoka kwenda Yerusalemu. 16 Baadhi ya waamini kutoka Kaisaria waliongozana nasi, wakat upeleka nyumbani kwa Mnasoni, mtu wa Kipro, mmoja wa waamini wa zamani, tukae kwake.

Taarifa Ya Paulo Kwa Kanisa La Yerusalemu

17 Tulipofika Yerusalemu ndugu wa huko walitukaribisha kwa furaha. 18 Kesho yake Paulo alikwenda nasi kwa Yakobo, na wazee wote wa kanisa walikuwepo. 19 Baada ya kuwasalimu, Paulo alitoa taarifa kamili ya mambo yote ambayo Mungu alifanya kati ya watu wa mataifa kwa kumtumia yeye. 20 Baada ya maelezo yake wote walimtukuza Mungu. Ndipo wakamwambia, “Unavyoona ndugu, kuna maelfu ya Wayahudi walioamini; nao wote wanaishika sheria kwa bidii. 21 Lakini wamekuwa wakiambiwa habari zako kuwa wewe umew afundisha Wayahudi wanaoishi na watu wa mataifa waache kushika sheria za Musa; na kuwaambia wasitahiri watoto wao, au kufuata mila za Kiyahudi. 22 Sasa tufanyeje? Kwa maana watasikia kwamba umefika Yerusalemu. 23 Kwa hiyo fanya kama tunavyokushauri. Tunao watu wanne hapa ambao wameweka nadhiri. 24 Wachukue hawa ukajitakase pamoja nao na ulipe gharama zao ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unashika sheria. 25 Lakini wale watu wa mataifa walioamini tumewapelekea barua tukiwaambia kuwa tumeamua wajitenge na kitu cho chote ambacho kimetolewa kwanza kama sadaka kwa miungu ya sanamu na wasinywe damu au kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa kunyongwa. Tena ni lazima wajitenge na uasherati.” 26 Kwa hiyo Paulo akawachukua wale watu na kesho yake akajita kasa pamoja nao. Akaingia ndani ya Hekalu ili akatoe taarifa ya tarehe ambayo siku zao za utakaso zitamalizika na sadaka kutolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.

Paulo Akamatwa

27 Zile siku saba zilipokaribia kumalizika, Wayahudi kutoka jimbo la Asia waliokuwa wamemwona Paulo ndani ya hekalu, waka chochea umati mkubwa wa watu wakamkamata Paulo. 28 Wakapiga kelele wakasema, “Ndugu Waisraeli, tusaidieni! Huyu ni yule mtu ambaye anafundisha watu kila mahali wawadharau watu wetu, wazid harau sheria zetu na hata hili Hekalu. Zaidi ya hayo amewaleta Wagiriki katika Hekalu na kuchafua hapa mahali patakatifu!” 29 Walisema hivi kwa sababu walimwona Trofimo, mwenyeji wa Efeso, akiwa mjini na Paulo wakadhani kuwa Paulo alikuwa amemleta Hekaluni . 30 Habari hizi zikawachochea watu wa mji mzima nao wakakimbia pamoja kwa hasira wakamkamata Paulo wakamtoa nje ya Hekalu. Milango ya Hekalu ikafungwa. 31 Walipokuwa wakitaka kum wua, habari zikamfikia Jemadari wa jeshi la askari wa Kirumi kwamba Yerusalemu yote ilikuwa katika hali ya machafuko. 32 Na mara yule jemadari akachukua maofisa wengine wa jeshi pamoja na maaskari wakakimbilia kwenye ile ghasia. Watu walipomwona jema dari na askari wakija, waliacha kumpiga Paulo. 33 Kisha yule jemadari akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani na alikuwa amefanya nini. 34 Baadhi ya watu wakapiga kelele wakieleza jambo moja na wengine wakieleza jingine. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata ukweli kamili kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi. 35 Basi walipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe Paulo juu juu kwa sababu ya fujo za ule umati wa watu 36 ambao walikuwa wakiwafuata wakipiga kelele, “Mwueni!”

Paulo Anajitetea

37 Walipokuwa wanakaribia kuingia katika ngome ya jeshi, Paulo alimwuliza yule jemadari, “Je, naweza kusema jambo moja?” Yule jemadari akajibu, “Kumbe unajua Kigiriki? 38 Wewe si yule Mmisri ambaye siku za karibuni alianzisha uasi akaongoza majam bazi elfu nne wenye silaha jangwani?” 39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso, jimbo la Kilikia na raia wa mji wenye sifa. Tafadhali niruhusu nizungumze na hawa watu.” 40 Yule jemadari alipomruhusu azungumze, Paulo akasimama penye ngazi akawapungia watu mkono ili wanyamaze. Watu walipokuwa kimya kabisa, Paulo akazungumza nao kwa lugha ya Kiebrania, akasema;

Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu

22 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakatulia zaidi, naye akasema, “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kili kia, lakini nimekulia hapa Yerusalemu, nikiwa mwanafunzi wa Gamalieli. Nilielimishwa kwa kufuata utaratibu maalumu wa sheria za baba zetu, nikiwa na ari ya kumheshimu Mungu kama ninyi mlivyo siku hii ya leo. Niliwatesa wafuasi wa ‘Njia’ mpaka wakafa. Niliwakamata, waume kwa wake, nikawafunga na kuwaweka gerezani. Kuhani mkuu na baraza zima la wazee ni mashahidi wangu kuhusu jambo hili. Wao ndio walionipa barua za kupeleka kwa ndugu zao huko Dameski. Kwa hiyo nilikwenda kuwakamata wafuasi wa ‘Njia’ niwalete Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. Nilipokuwa nimekaribia kufika Dameski, mnamo muda wa kama saa sita mchana, kulitokea mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza pande zote kuni zunguka. Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’ Naye akajibu, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’

“Wale watu niliokuwa nikisafiri nao waliona ule mwanga, lakini hawakuelewa ile sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10 Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’ Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski na huko utaambiwa mambo yote uliyopangiwa kufanya.’ 11 Nilikuwa sioni kwa sababu ya ule mwanga mkali kwa hiyo wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza na hivyo tukafika Dameski. 12 “Mtu mmoja aitwaye Anania, mtu wa dini, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi wote wa Dameski, 13 alinijia akasimama karibu yangu akasema, ‘Ndugu Sauli, pokea tena uwezo wa kuona!’ Na wakati ule ule nikaweza kuona tena, nikamwona Anania. 14 Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake, umwone yeye Mwenye Haki na usikie akisema nawe kwa sauti yake mwenyewe. 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu wote uwaambie yote uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, mbona unakawia? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako kwa kuliitia jina lake.” ’

Wito Wa Paulo Kuwahubiri Mataifa

17 “Niliporudi Yerusalemu nikawa naomba Hekaluni 18 nilim wona katika ndoto akiniambia ‘Harakisha uondoke Yerusalemu upesi kwa sababu watu hawa hawatakubali ushuhuda wako juu yangu.’ 19 Nikajibu, ‘Bwana, wanajua jinsi nilivyokuwa nikienda katika masinagogi nikawafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini wewe. 20 Na hata shahidi wako Stefano alipokuwa anauawa mimi nilikuwa nimesimama kando nikikubaliana na kitendo hicho na nikashika mavazi ya wale waliomwua. 21 Akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa mataifa.”

22 Watu walimsikiliza Paulo mpaka hapo; kisha wakapaaza tena sauti zao wakasema, “Mwondosheni duniani! Mtu kama huyu hasta hili kuishi!” 23 Walipoendelea kupiga kelele na kupeperusha nguo zao na kutupa mavumbi juu hewani, 24 yule jemadari akaamuru wale askari wake wamwingize Paulo katika ngome na wamhoji na kum chapa viboko ili aeleze vizuri kwa nini wale Wayahudi walikuwa wanampigia makelele. 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia askari aliyekuwa karibu naye, “Je, ni halali kumpiga raia wa Kirumi kabla hajahu kumiwa kwa kosa lo lote?” 26 Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari akamwuliza, “Unajua unalolifanya? Huyu mtu ni raia wa Kirumi.” 27 Kwa hiyo yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Kirumi?” Paulo aka jibu, “Ndio.” 28 Yule jemadari akasema, “Mimi nilinunua uraia wangu kwa fedha nyingi.” Paulo akamjibu, ‘ ‘Lakini mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.” 29 Wale wote waliokuwa wamejiandaa kumhoji wakaondoka haraka haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, kwa maana alitambua ya kuwa alikuwa amemfunga raia wa Kirumi kinyume cha sheria.

Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza

30 Kesho yake yule jemadari alimfungua Paulo zile kamba ali zofungwa akaamuru makuhani wakuu na baraza lote likutane. Akamleta Paulo mbele yao ili apate kujua kwa nini Wayahudi wali kuwa wanamshtaki.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica

  Back

1 of 1

You'll get this book and many others when you join Bible Gateway Plus. Learn more

Viewing of
Cross references
Footnotes