Font Size
Yohana 15:2-4
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yohana 15:2-4
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Yeye hulikata kutoka kwangu kila tawi lisilozaa matunda.[a] Pia hupunguza majani katika kila tawi linalozaa matunda ili kuliandaa liweze kuzaa matunda zaidi. 3 Ninyi mmewekwa tayari[b] kwa ajili ya kuzaa matunda[c] kutokana na mafundisho yale niliyowapa. 4 Hivyo mkae mkiwa mmeunganishwa kwangu, nami nitakaa nikiwa nimeunganishwa kwenu. Hakuna tawi linaloweza kuzaa matunda likiwa liko peke yake. Ni lazima liwe limeunganishwa katika mzabibu. Ndivyo ilivyo hata kwenu. Hamwezi kutoa matunda mkiwa peke yenu. Ni lazima muwe mmeunganishwa kwangu.
Read full chapterFootnotes
- 15:2 lisilozaa matunda Kuzaa matunda inamaanisha jinsi wafuasi wa Yesu wanavyopaswa kuishi ili kuonesha kuwa wao ni wa Yesu. Tazama mstari wa 7-10.
- 15:3 mmewekwa tayari Ni kufanywa safi kwa njia ya kukatiwa matawi (Kiyunani “Kusafishwa”) ilivyoelezwa kwenye mstari wa 2.
- 15:3 kuzaa matunda Ni jinsi wafuasi wa Yesu wanavyopaswa kuwa ili kudhihirisha kuwa wao ni wa Yesu.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International