Yesu Anawaombea Wanafunzi Wake

17 Yesu alipomaliza kusema maneno haya, alitazama mbinguni akasema, “Baba, wakati umefika. Dhihirisha utukufu wangu ili nami nikutukuze wewe, kwa kuwa umenipa mamlaka juu ya watu wote, niwape uzima wa milele wale ambao umewakabidhi kwangu. Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfah amu Yesu Kristo ambaye umemtuma. Baba nime kutukuza hapa duniani kwa kutimiza kazi uliyonipa niifanye. Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa. Nimewafahamisha jina lako wale ambao umenipa kutoka katika ulimwengu. Wao wametii neno lako. Sasa wamefahamu ya kuwa vyote ulivyonipa vinatoka kwako ; kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma. Siwaombei watu wote wa ulimwengu bali nawaombea hawa ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote ulionipa ni wako, na walio wako ni wangu; nao wanadhihirisha utukufu wangu. 11 Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwalinda wakawa salama kwa uwezo wa jina ulilonipa. Nimewalinda na hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyeamua kupotea, ili Maandiko yapate kutimia. 13 Lakini sasa nakuja kwako na ninasema haya wakati nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kikamil ifu. 14 Nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao, kama mimi, si wa ulimwengu huu. 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu shetani. 16 Kama mimi nisivyo mwenyeji wa ulimwengu huu, wao pia sio wa ulimwengu. 17 Watakase kwa neno lako; kwa maana neno lako ndilo kweli. 18 Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma wao ulim wenguni. 19 Kwa ajili yao nimejitoa wakfu kwako ili na wao wapate kuwa watakatifu kwa kufahamu kweli yako.

Yesu Anawaombea Watakaoamini Baadaye

20 “Siwaombei hawa peke yao; bali nawaombea pia wale wote watakaoniamini kwa sababu ya ushuhuda wa hawa. 21 Ninawaombea wote wawe kitu kimoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi ni ndani yako; ili na wao wawe ndani yetu na ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ulinituma. 22 Nimewapa utukufu ule ule ulionipa ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo - 23 mimi nikiwa ndani yao na wewe ndani yangu; ili wakamilike katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma na kwamba unawapenda kama unavyonipenda mimi. 24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimekutambulisha wewe kwao, na nitaendelea kulitambulisha jina lako kwao ili upendo ulio nao kwangu uwe upendo wao pia; nami niwe ndani yao.”

Yesu Aomba Kwa ajili Yake na Wafuasi Wake

17 Baada ya Yesu kusema maneno hayo, alitazama mbinguni na kuomba, “Baba, wakati umefika. Mpe utukufu Mwanao ili Mwanao naye akupe wewe utukufu. Ulimpa Mwana mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wale wote uliompa. Na uzima wa milele ndiyo huu: kwamba watu watakujua wewe, Mungu pekee wa kweli, na kwamba watamjua Yesu Kristo, Yeye uliyemtuma. Mimi nimeimaliza kazi uliyonipa niifanye. Nami nimekupa utukufu duniani. Sasa, Bwana, unipe utukufu wako niwe nao pamoja nawe, utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuumbwa ulimwengu.

Wewe ulinipa baadhi ya wafuasi kutoka watu wa ulimwengu huu. Hao nimewaonesha jinsi wewe ulivyo. Walikuwa watu wako, lakini ukawakabidhi kwangu. Wao wameyashika mafundisho yako. Sasa wanajua kuwa kila kitu nilichonacho kimetoka kwako. Mimi niliwaeleza maneno uliyonipa, nao wakayapokea. Walitambua ukweli kuwa mimi nilitoka kwako na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma. Mimi ninawaombea hao sasa. Siwaombei watu walioko ulimwenguni. Bali nawaombea wale watu ulionipa, kwa sababu hao ni wako. 10 Vyote nilivyo navyo ni vyako, na vyote ulivyo navyo ni vyangu. Kisha utukufu wangu umeonekana ndani yao.

11 Sasa nakuja kwako. Mimi sitakaa ulimwenguni, lakini hawa wafuasi wangu bado wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu, uwaweke hao salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Ndipo watapokuwa na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Niliwalinda. Ni mmoja wao tu aliyepotea; yule ambaye kwa hakika angelikuja kupotea. Hii ilikuwa hivyo ili kuonesha ukweli wa yale yaliyosemwa na Maandiko kuwa yangetokea.

13 Nami nakuja kwako sasa. Lakini maneno haya nayasema ningali nimo ulimwenguni ili wafuasi hawa wawe na furaha kamili ndani yao. 14 Nimewapa mafundisho yako. Nao ulimwengu umewachukia, kwa sababu wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu.

15 Siombi kwamba uwaondoe katika ulimwengu. Bali ninaomba uwalinde salama kutoka kwa Yule Mwovu.[a] 16 Wao si wa ulimwengu huu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu huu. 17 Kupitia kweli yako uwatayarishe kwa utumishi wako. Mafundisho yako ndiyo kweli. 18 Mimi nimewatuma ulimwenguni, kama wewe ulivyonituma mimi ulimwenguni. 19 Nami najiweka tayari kabisa kukutumikia wewe. Ninafanya hivi kwa ajili yao ili wao nao wawe wamekamilika kukutumikia.

20 Siwaombei tu hao wafuasi wangu lakini nawaombea pia wale watakaoniamini kutokana na mafundisho yao. 21 Baba, naomba kwamba wote wanaoniamini waungane pamoja na kuwa na umoja. Wawe na umoja kama vile wewe na mimi tulivyoungana; wewe umo ndani yangu nami nimo ndani yako. Nami naomba nao pia waungane na kuwa na umoja ndani yetu. Ndipo ulimwengu nao utaamini kuwa ndiwe uliyenituma. 22 Mimi nimewapa utukufu ule ulionipa. Nimewapa utukufu huo ili wawe na umoja, kama mimi na wewe tulivyo na umoja. 23 Nitakuwa ndani yao, nawe utakuwa ndani yangu. Hivyo watakuwa na umoja kamili. Kisha ulimwengu utajua kwamba wewe ndiwe uliyenituma na ya kuwa uliwapenda jinsi ulivyonipenda mimi.

24 Baba, ninataka hawa watu ulionipa wawe nami mahali pale nitakapokuwa. Nataka wauone utukufu wangu, utukufu ule ulionipa kwa sababu ulinipenda kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba wewe ndiye unayetenda yaliyo haki. Ulimwengu haukujui, bali mimi nakujua, na hawa wafuasi wangu wanajua kuwa wewe ndiye uliyenituma. 26 Nimewaonesha jinsi ulivyo, na nitawaonesha tena. Kisha watakuwa na upendo ule ule ulio nao wewe kwangu, nami nitaishi ndani yao.”

Footnotes

  1. 17:15 Mwovu Ni Shetani au Ibilisi.