Kwa sababu hii, mimi Paulo, nimekuwa mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu wa mataifa. Ninaamini kwamba mmek wisha sikia kuwa Mungu amenipa neema yake niwe mhudumu kwa ajili yenu; na kwamba Mungu alinifahamisha siri hii kwa njia ya mafu nuo, kama nilivyokwisha andika kwa kifupi. Kwa hiyo mtakaposoma barua hii mtaweza kutambua ufahamu niliopewa kuhusu siri ya Kris to. Siri hii haikufahamika kwa watu wa vizazi vilivyopita kama ilivyodhihirishwa sasa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa mataifa ni warithi pamoja na Waisraeli; na wote pamoja ni viungo vya mwili mmoja, na ni washiriki kwa pamoja wa ile ahadi aliyotoa Mungu katika Kristo Yesu. Niliteuliwa kuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa uwezo wake uliokuwa ukifanya kazi ndani yangu. Ingawa mimi ni mdogo kuliko hata aliye mdogo kabisa kati ya watu wote wa Mungu, nilipewa neema hii, niwahubirie watu wa mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo. Na nieleze wazi wazi ili watu wote waone jinsi siri hii itakavyotekelezwa. Siri hii ilikuwa imefichwa tangu awali kwa Mungu aliyeumba vitu vyote. 10 Yeye alikusudia kwamba sasa, kwa njia ya kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kufa hamika kwa mamlaka na nguvu zote katika makao ya mbinguni. 11 Mpango huu ulikuwa sawasawa na mapenzi yake yaliyotimi zwa katika Kristo Yesu Bwana wetu, 12 ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia Mungu kwa njia ya imani katika Kristo. 13 Kwa hiyo, nawasihi msikate tamaa kutokana na mateso ninayopata kwa ajili yenu; mateso haya ni utukufu wenu. Sala Ya Paulo Kwa Waefeso

14 Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, 15 aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; 19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. 20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. 21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.

Huduma ya Paulo kwa Wasio Wayahudi

Hivyo, mimi Paulo ni mfungwa kwa sababu ninamtumikia Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi msio Wayahudi. Mnajua hakika ya kuwa Mungu alinipa kazi hii kupitia neema yake ili niwasaidie. Mungu alinionyesha na nikaweza kuujua mpango wake wa siri. Nimekwisha kuandika kiasi fulani juu ya hili. Na ikiwa mtasoma nilichowaandikia, mtajua kuwa ninaielewa siri ya kweli kuhusu Kristo. Watu walioishi zamani hawakuambiwa siri hiyo. Lakini sasa, kupitia Roho, Mungu amewawezesha mitume na manabii wake watakatifu kuijua siri hiyo. Na siri hiyo ni hii: Kwa kuikubali Habari Njema, wale wasio Wayahudi watashiriki pamoja na Wayahudi katika baraka alizonazo Mungu kwa ajili ya watu wake. Wao ni sehemu ya mwili mmoja, na wanashiriki manufaa ya ahadi ambayo Mungu aliitimiza kupitia Kristo Yesu.

Kwa kipawa cha neema ya Mungu, nilifanywa mtumishi wa kuihubiri Habari Njema. Alinipa neema hiyo kwa nguvu zake. Mimi nisiye na umuhimu zaidi miongoni mwa watu wa Mungu. Lakini alinipa kipawa hiki cha kuwahubiri wasio Wayahudi Habari Njema kuhusu utajiri alionao Kristo. Utajiri huu ni mkuu na si rahisi kuuelewa kikamilifu. Pia Mungu alinipa kazi ya kuwaambia watu kuhusu mpango wa siri yake ya kweli. Aliificha siri hii ya kweli ndani yake tangu mwanzo wa nyakati. Ndiye aliyeumba kila kitu. 10 Lengo lake lilikuwa kwamba watawala wote na mamlaka zote zilizo mbinguni zijue njia nyingi anazotumia kuionesha hekima yake. Watalijua hili kwa sababu ya kanisa. 11 Hii inaendana na mpango aliokuwa nao Mungu tangu mwanzo wa nyakati. Alitekeleza mpango wake kupitia Kristo Yesu Bwana wetu. 12 Kwa kuwa tu wake Kristo tunakuja mbele za Mungu tukiwa huru bila woga. Tunaweza kufanya hivi kwa sababu ya uaminifu wake Kristo.[a] 13 Hivyo ninawaomba msikate tamaa kutokana na yale yanayonipata. Mateso yangu ni faida kwenu, na pia ni kwa ajili ya heshima na utukufu wenu.

Upendo wa Kristo

14 Hivyo ninapiga magoti nikimwomba Baba. 15 Ambaye katika yeye kila familia iliyoko mbinguni na duniani inapewa jina. 16 Ninamwomba Baba kwa kadri ya utajiri wa utukufu wake awajaze nguvu za ndani kwa nguvu za Roho wake. 17 Ninaomba kwamba Kristo aishi katika mioyo yenu kwa sababu ya imani yenu. Ninaomba maisha yenu yawe na mizizi mirefu na misingi imara katika upendo. 18 Na ninaomba ili ninyi na watakatifu wote wa Mungu muwe na uwezo wa kuuelewa upana, urefu, kimo na kina cha ukuu wa upendo wa Kristo. 19 Upendo wa Kristo ni mkuu kuliko namna ambavyo mtu yeyote anaweza kujua, lakini ninawaombea ili mweze kuujua. Ndipo mtajazwa kwa kila kitu alichonacho Mungu kwa ajili yenu.

20 Tukiwa na nguvu za Mungu zinazotenda kazi ndani yetu, anaweza kufanya zaidi, zaidi ya kila kitu tunachoweza kuomba au kufikiri. 21 Atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kila wakati, milele na milele. Amina.

Footnotes

  1. 3:12 uaminifu wake Kristo Au “kwa sababu ya imani katika Kristo”.