Hati Na Mwana-Kondoo

Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwe nye kile kiti cha enzi hati iliyoandikwa ndani na nje, ambayo ilikuwa imefungwa na mihuri saba. Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, “Ni nani anayestahili kufungua hati hii na kuvunja mihuri yake?” Lakini hakupatikana mtu mbinguni, juu ya nchi, wala chini ya nchi aliyeweza kufungua hati hiyo, wala kuitazama. Nililia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kuifungua hati hiyo wala kuitazama. Kisha, mmoja wapo wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, yule simba wa kabila la Yuda, wa ukoo wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kufun gua hati hiyo na kuvunja mihuri yake saba.” Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote . Huyo Mwana-Kondoo akaenda, akaichukua ile hati kutoka kwenye mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za mal aika wengi sana wakizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi ya hao mal aika ilikuwa ni maelfu na maelfu na kumi elfu mara kumi elfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, “Mwana -Kondoo aliyeuawa anasta hili kupewa uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima, na utukufu na sifa!” 13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, juu ya nchi na chini ya nchi, baharini na vyote vilivy omo baharini wakiimba, “Baraka na heshima na utukufu na uweza ni wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi; na kwa Mwana-Kondoo, hata milele na milele! 14 Na wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.