Menu
Bible Gateway Plus logo
Bible Gateway logo
account
Welcome to the new Bible Gateway. Take a quick tour and see what’s new.
Bible Gateway Plus logo
Bible Gateway logo
Verse of the Day by email. Sign up free.
  • Read
    • Reading Plans
    • Advanced Search
    • Available Versions
    • Audio Bibles
  • Study
    • Scripture Engagement
    • More Resources
  • News
  • Explore
    • Newsletters
    • Devotionals
    • Bible Gateway App
    • Bible Audio App
    • Take a Tour
  • Store
    • Bibles
    • Deals
    • More
  • Bible Gateway Plus
SNT
Version
Bible Books Bible Books
SNT
Version
Read
Study
News
Explore
Store
Bible Gateway Plus
Light Mode Dark Mode
Font Size
Log In show menu
Previous Next
Listen to Tito 1AudioPrint PrintSettingsSettingsShare ShareParallelParallelExpandExpandCollapse

Tito 1  Neno: Bibilia Takatifu

1 Kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo. Mimi nimetumwa kwa wale ambao Mungu amewateua ili niwaon goze katika imani na katika maarifa ya kweli yanayopatana na kum cha Mungu; 2 na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo. 3 Naye kwa wakati aliopanga alidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo nilikabidhiwa kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.

4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu

Kazi Ya Tito Kule Krete

5 Nilikuacha huko Krete kusudi urekebishe mambo yote yal iokuwa hayakunyooka na uchague wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na lawama yo yote; awe mume wa mke mmoja; awe ni mtu ambaye watoto wake ni waamini na wala sio jeuri au wasiotii. 7 Kwa kuwa askofu amekabidhiwa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na lawama. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyokuwa ya halali. 8 Bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye kujitawala, mnyofu, mtakatifu na mwe nye kudhibiti na si yake. 9 Ni lazima alishike kwa uthabiti neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine na kudhihirisha makosa ya wale wanaolipinga.

Walimu Wa Uongo

10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.

16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.

Next
2 Timotheo 4
Tito 2
Next
dropdown
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica

Bible Gateway Plus logo
Bible Gateway logo

Font Size

Font Size

Dark Mode

Light Mode Dark Mode

About

  • About
  • Learn About the Bible
  • Statement of Faith
  • Mobile App
  • Store
  • Blog
  • Newsroom
  • Support Us

Help

  • FAQs
  • Tutorials
  • Use Bible Gateway on Your Site
  • Advertise with us
  • Contact us
  • Privacy policy
  • California Privacy Rights
  • Do Not Sell My Personal Information
  • Site: Terms of use
  • Widget: Terms of use

Our Network

  • FaithGateway
  • StudyGateway
  • ChurchSource
  • HarperCollins Christian Publishing
  • Grupo Nelson
  • Editorial Vida
  • Thomas Nelson
  • WestBow Press
  • Zondervan
  • MasterLectures

Social

  • Facebook
  • Instagram
  • Pinterest
  • TikTok
  • X
  • YouTube

Preferences

  • Versión en español
  • Preferences
  • Classic Bible Gateway
Sign Up for Bible Gateway: News & Knowledge
Get weekly Bible news, info, reflections, and deals in your inbox.

By submitting your email address, you understand that you will receive email communications from Bible Gateway, operated by HarperCollins Christian Publishing, 501 Nelson Pl, Nashville, TN 37214 USA, including commercial communications and messages from partners of Bible Gateway. You may unsubscribe from Bible Gateway’s emails at any time. If you have any questions, please review our Privacy Policy or email us at privacy@biblegateway.com.

Preferences

  • Versión en español
  • Preferences
  • Classic Bible Gateway