Dalili Za Siku Za Mwisho

24 Yesu aliondoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wana funzi wakamwendea ili wakamwonyeshe majengo ya Hekalu. Lakini yeye akawaambia, “Mnayaona haya yote? Nawaambieni kweli, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, yote yatatupwa chini.”

Yesu alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni wanafunzi wake walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tueleze, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kuja kwako na mwisho wa dunia?”

Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu asije akawadanganya. Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema, ‘Mimi ndiye Kristo’ nao watawapotosha wengi. Mtasikia habari za vita na tetesi za vita, msitishike; kwa maana haya hayana budi kutokea; lakini mwisho utakuwa bado. Taifa kwa taifa na nchi kwa nchi zitapigana. Kutakuwa na njaa na tetemeko la ardhi sehemu mbalim bali. Haya yote yatakuwa kama mwanzo wa uchungu wa uzazi.

“Kisha mtasalitiwa, mtateswa na kuuawa na mtachukiwa na watu wa mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Wakati huo, wengi wataacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana, 11 na watatokea manabii wengi wa uongo ambao watawapotosha watu. 12 Kwa sababu uovu utakuwa umeenea sana, upendo wa watu wengi utapoa. 13 Lakini mtu atakayesimama imara mpaka mwisho, ataoko lewa. 14 Na hii Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kama ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utafika.

15 “Mtakapoona lile ‘Chukizo la Uharibifu’ linalozungumzwa na nabii Danieli limesimama mahali Patakatifu - msomaji na aelewe - 16 basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 17 Aliyeko juu ya nyumba asishuke kuchukua vitu vyake ndani. 18 Aliyeko sham bani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 19 Ole wao wanawake watakaokuwa na mimba na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ili mtakapokuwa mnakimbia, isiwe ni kipindi cha baridi au siku ya sabato. 21 Kwa maana kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa na ambayo haitatokea tena. 22 Kama siku hizo zisingepunguzwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angesalimika, lakini kwa ajili ya wale walioteu liwa na Mungu, siku hizo zitapunguzwa. 23 Wakati huo mtu aki waambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa!’ au ‘Kristo yule pale!’ msi sadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu. 25 Angalieni, nawatahadharisha mapema.

26 “Kwa hiyo wakiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msitoke. Au wakisema, ‘Yuko chumbani 27 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea mashariki na kuangaza mpaka magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwangu mimi Mwana wa Adamu. 28 Kwa maana po pote ulipo mzoga, ndipo wakusanyikapo tai.

29 “Mara baada ya dhiki ya wakati huo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake tena, na nyota zitaanguka kutoka mbin guni; nguvu za anga zitatikisika. 30 Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu angani na watu wote ulimwenguni wataomboleza. Nao wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 31 Na nitawatuma malaika zangu kwa sauti kuu ya tarumbeta na watawakusanya wateule wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

32 “Jifunzeni kutoka kwa mti wa mtini. Matawi yake yana poanza kuwa laini na majani kuchipua, mnafahamu kwamba kiangazi kimekaribia. 33 Basi, pia mkiona dalili hizi, fahamuni kwamba amekaribia kurudi, na yu karibu na mlango. 34 Nawaambieni kweli, hakika kizazi hiki hakitapita kabla mambo haya hayajatokea. 35 Mbingu na dunia zitatoweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

36 “Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni wala Mwana, isipokuwa Baba peke yake. 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.

40 “Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 41 Wanawake wawili watakuwa wanatwanga; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa.

42 “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani ataka pokuja Bwana wenu.

43 “Lakini fahamuni kwamba, kama mwenye nyumba angalifahamu ni saa ngapi za usiku ambapo mwizi atakuja, angalikaa macho asiache nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo ninyi pia lazima muwe tayari kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja saa ambayo hamnita zamii.”

Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu

45 “Basi, ni nani mtumishi mwaminifu ambaye bwana wake amemweka awe msimamizi wa watumishi wengine nyumbani kwake, awape posho yao kwa wakati wake? 46 Heri mtumishi ambaye atakapokuja bwana wake atamkuta anafanya hivyo. 47 Nawaambieni kweli, atam fanya mtumishi huyo asimamie mali yake yote.

48 “Lakini kama mtumishi huyo ni mwovu atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu hatarudi kwa muda mrefu,’ 49 na ataanza kuwapiga watumishi wenzake na kula na kunywa na walevi. 50 Bwana wake atakuja wakati ambapo mtumishi huyo hamtazamii na saa ambayo haijui. 51 Ndipo atamwadhibu huyo mtumishi na kumweka katika kundi la wanafiki; huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.”