21 Alipokuwa Hekaluni Yesu aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la sadaka. Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”

Dalili Za Siku Za Mwisho

Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuhusu Hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na mapambo maridadi yaliyotolewa kama sadaka kwa Mungu. Yesu akawaambia, “Wakati unakuja ambapo vyote hivyo mnavyovistaajabia sasa vitabomolewa, halitabaki hata jiwe moja juu ya jingine.” Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakari bia?” Akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja wakitumia jina langu, na kusema, ‘Mimi ndiye’ na ‘Wakati umekaribia’. Msiwafuate. Na mtakaposikia habari za vita na machafuko, msiogope, kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila mwisho hautatokea wakati huo.”

10 Kisha akawaambia: “Taifa moja litapigana na taifa lin gine na utawala mmoja utapigana na utawala mwingine. 11 Kutaku wepo na matetemeko ya ardhi, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali; kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.”

Mateso

12 “Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13 Na hii itawapa nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu imani yenu. 14 Lakini msiwe na wasiwasi juu ya matayarisho ya utetezi wenu kabla ya mashtaka. 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo maadui zenu hawa taweza kukataa au kupinga. 16 Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu mtauawa. 17 Watu wote watawa chukia kwa ajili yangu. 18 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! 19 Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.”

Kuteketezwa Kwa Yerusalemu

20 “Mkiona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, faham uni kwamba karibu utaangamizwa. 21 Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani; walio mjini Yerusalemu waondoke humo na wale walioko mashambani wasije mjini. 22 Kwa sababu huu utakuwa wakati wa kulipiza kisasi ili yale yote yaliyosemwa kwenye Maan diko yatimie.

23 “Ole wao akina mama watakaokuwa waja wazito na wata kaokuwa wakinyonyesha! Kutakuwa na dhiki nchini na ghadhabu ya Mungu itakuwa juu ya watu wa taifa hili. 24 Wengine watauawa kwa silaha na wengine watachukuliwa mateka na kupelekwa nchi mbalim bali. Na Yerusalemu itamilikiwa na watu wa mataifa mengine mpaka muda wa mataifa hayo utakapokwisha.”

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

25 “Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26 Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27 Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. 28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”

29 Akawaambia mfano, “Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Inapochipua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu. 31 Hali kadhalika, mkiyaona mambo haya yanatokea, faham uni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitakwisha kabla mambo haya hayajatokea. 33 Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.” Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla

34 Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35 Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36 Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”

37 Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni na jioni ili pofika alikwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. 38 Na asubuhi na mapema watu wote walikuwa wakija Hekaluni kumsikiliza.

Mjane Aonesha Jinsi Ulivyo Utoaji wa Kweli

(Mk 12:41-44)

21 Yesu alitazama na kuwaona matajiri wakimtolea Mungu sadaka zao katika sanduku la sadaka ndani ya Hekalu. Kisha akamwona mjane maskini akiweka sarafu mbili za shaba kwenye sanduku. Akasema, “Mjane huyu maskini ametoa sarafu mbili tu. Lakini ukweli ni kuwa, ametoa zaidi ya hao matajiri wote. Wale wanavyo vingi, na wametoa vile ambavyo hawavihitaji. Lakini mwanamke huyu ni maskini sana, lakini ametoa vyote alivyokuwa akitegemea ili aishi.”

Yesu Aonya Kuhusu Wakati Ujao

(Mt 24:1-14; Mk 13:1-13)

Baadhi ya watu walikuwa wanazungumza kuhusu uzuri wa Hekalu lililojengwa kwa mawe safi na kupambwa kutokana na matoleo mbalimbali ambayo watu humtolea Mungu ili kutimiza nadhili zao.

Lakini Yesu akasema, “Wakati utafika ambao yote mnayoyaona hapa yatateketezwa. Kila jiwe katika majengo haya litatupwa chini. Hakuna jiwe litakaloachwa juu ya jingine.”

Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Dalili ipi itatuonyesha kwamba ni wakati wa mambo haya kutokea?”

Yesu akasema, “Iweni waangalifu, msije mkarubuniwa. Watu wengi watakuja wakitumia jina langu, watasema, ‘Mimi ndiye Masihi,’[a] na ‘Wakati sahihi umefika!’ Lakini msiwafuate. Mtakaposikia kuhusu vita na machafuko, msiogope. Mambo haya lazima yatokee kwanza. Lakini mwisho hautakuja haraka.”

10 Kisha Yesu akawaambia, “Mataifa yatapigana na mataifa mengine. Falme zitapigana na falme zingine. 11 Kutakuwa matetemeko makubwa, kutakuwa njaa na magonjwa ya kutisha sehemu nyingi. Mambo ya kutisha yatatokea, na mambo ya kushangaza yatatokea kutoka mbinguni ili kuwaonya watu.

12 Lakini kabla ya mambo haya yote kutokea, watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawahukumu katika masinagogi yao na kuwafunga gerezani. Mtalazimishwa kusimama mbele ya wafalme na magavana. Watawatendea mambo haya yote kwa sababu ninyi ni wafuasi wangu. 13 Lakini hili litawapa ninyi fursa ya kuhubiri juu yangu. 14 Msihofu namna mtakavyojitetea, 15 Nitawapa hekima kusema mambo ambayo adui zenu watashindwa kuyajibu. 16 Hata wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa, na marafiki watawageuka. Watawaua baadhi yenu. 17 Kila mtu atawachukia kwa sababu mnanifuata mimi. 18 Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea. 19 Mtayaokoa maisha yenu ikiwa mtaendelea kuwa imara katika imani mnapopita katika mambo haya yote.

Kuharibiwa Kwa Mji wa Yerusalemu

(Mt 24:15-21; Mk 13:14-19)

20 Mtakapoona majeshi yameuzunguka mji wa Yerusalemu, ndipo mtajua kuwa wakati wa kuharibiwa kwake umefika. 21 Watu walioko katika Uyahudi wakati huo wakimbilie milimani. Mtu yeyote atakaye kuwa Yerusalemu wakati huo aondoke haraka. Ikiwa utakuwa karibu na mji, usiingie mjini! 22 Manabii waliandika mambo mengi kuhusu wakati ambao Mungu atawaadhibu watu wake. Wakati ninaouzungumzia ni wakati ambao mambo haya yote lazima yatokee. 23 Wakati huu utakuwa mgumu kwa wanawake wenye mimba au wanaonyonyesha watoto wadogo, kwa sababu mambo mabaya yatakuja katika nchi hii. Mungu atawaadhibu watu wake kwa sababu wamemkasirisha. 24 Baadhi ya watu watauawa, wengine watafanywa watumwa na kuchukuliwa katika nchi mbalimbali. Mji mtakatifu wa Yerusalemu utatekwa na kuwekwa chini ya utawala wa wageni mpaka wakati ulioruhusiwa wao kufanya hivi utakapokwisha.

Msiogope

(Mt 24:29-31; Mk 13:24-27)

25 Mambo ya kushangaza yatatokea kwenye jua, mwezi na nyota na watu katika dunia yote wataogopa na kuchanganyikiwa kutokana na kelele za bahari na mawimbi yake. 26 Watazimia kwa hofu na kuogopa watakapoona mambo yanayoupata ulimwengu. Kila kitu katika anga kitabadilishwa. 27 Kisha watu watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu mwenye nguvu na utukufu mwingi. 28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara na msiogope. Jueni kuwa wakati wa Mungu kuwaweka huru umekaribia!”

Maneno Yangu Yataishi Milele

(Mt 24:32-35; Mk 13:28-31)

29 Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Tazameni miti yote. Mtini ni mfano mzuri. 30 Unapochipua majani mnatambua kwamba majira ya joto yamekaribia. 31 Kwa namna hiyo hiyo, mtakapoona mambo haya yote yanatokea, mtajua kwamba ufalme wa Mungu umekaribia kuja.

32 Ninawahakikishia kwamba, wakati mambo haya yote yatakapotokea, baadhi ya watu wanaoishi sasa watakuwa hai bado. 33 Ulimwengu wote, dunia yote na anga vitapita, lakini maneno yangu yataishi milele.

Kuweni Tayari Wakati Wote

34 Iweni waangalifu, msiutumie muda wenu katika sherehe za ulevi na kuhangaikia maisha haya. Mkifanya hivyo, hamtaweza kufikiri vyema na mwisho unaweza kuja mkiwa hamjajiandaa. 35 Mwisho utakuja kwa kushitukiza kwa kila mtu duniani. 36 Hivyo, iweni tayari kila wakati. Ombeni ili muepuke mambo haya yote yatakayotokea na mweze kusimama kwa ujasiri mbele za Mwana wa Adamu.”

37 Wakati wa mchana Yesu aliwafundisha watu katika eneo la Hekalu. Usiku alitoka nje ya mji na kukaa usiku kucha kwenye kilima kinachoitwa Mlima wa Mizeituni. 38 Kila asubuhi watu wote waliamka mapema kwenda kumsikiliza Yesu katika Hekalu.

Footnotes

  1. 21:8 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Yule ambaye”, kwa maana ya Mfalme Mteule wa Mungu aliyetumwa na Mungu. Tazama Mt 24:5 na Masihi katika Orodha ya Maneno.