11 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. Utupatie chakula chetu kila siku. Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10 Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11 “Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12 Au akimwomba yai atampa nge? 13 Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho

Yesu Na Beelzebuli

14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.

24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”

27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”

Ishara Ya Yona

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 30 Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa. 31 Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa. 32 Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko

Taa Ya Mwili

33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”

Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria

37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja. 38 Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa. 39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.

42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.

43 “Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni! 44 Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

45 Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!” 46 Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza. 47 Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu. 48 Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.

49 “Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’ 50 Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki; 51 tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote. 52 Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”

53 Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi, 54 wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.

Yesu Afundisha Kuhusu Maombi

(Mt 6:9-15)

11 Siku moja Yesu alitoka akaenda mahali fulani kuomba. Alipomaliza, mmoja wa wafuasi wake akamwambia, “Yohana aliwafundisha wafuasi wake namna ya kuomba. Bwana, tufundishe nasi pia.”

Yesu akawaambia wafuasi wake, “Hivi ndivyo mnapaswa kuomba:

‘Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe daima.
    Tunaomba Ufalme wako uje.
Utupe chakula tunachohitaji kila siku.
Utusamehe dhambi zetu,
    kama tunavyomsamehe kila mtu anayetukosea.
Na usiruhusu tukajaribiwa.’”

Mwombeni Mungu Kile Mnachohitaji

(Mt 7:7-11)

5-6 Kisha Yesu akawaambia, “Chukulia mmoja wenu angekwenda kwa rafiki yake usiku na kumwambia, ‘Rafiki yangu aliyekuja mjini amekuja kunitembelea. Lakini sina chakula cha kumpa ili ale. Tafadhali nipe mikate mitatu.’ Rafiki yako ndani ya nyumba akajibu, ‘Nenda zako! Usinisumbue! Mlango umefungwa. Mimi na watoto wangu tumeshapanda kitandani kulala. Siwezi kuamka ili nikupe kitu chochote kwa sasa.’ Ninawaambia, urafiki unaweza usimfanye aamke akupe kitu chochote. Lakini hakika ataamka ili akupe unachohitaji ikiwa utaendelea kumwomba. Hivyo ninawaambia, Endeleeni kuomba na Mungu atawapa. Endeleeni kutafuta na mtapata. Endeleeni kubisha milangoni, na milango itafunguliwa kwa ajili yenu. 10 Ndiyo, kila atakayeendelea kuomba atapokea. Kila atakayeendelea kutafuta atapata. Na kila atakayeendelea kubisha mlangoni, mlango utafunguliwa kwa ajili yake. 11 Je, kuna mmoja wenu aliye na mwana? Utafanya nini ikiwa mwanao atakuomba samaki? Je, kuna baba yeyote anayeweza kumpa nyoka? 12 Au akiomba yai, utampa nge? Hakika hakuna baba wa namna hivyo. 13 Ikiwa ninyi waovu mnajua namna ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Vivyo hivo, hakika Baba yenu aliye mbinguni anajua namna ya kuwapa Roho Mtakatifu wale wanao mwomba?”

Nguvu ya Yesu Inatoka kwa Mungu

(Mt 12:22-30; Mk 3:20-27)

14 Wakati mmoja Yesu alikuwa akitoa pepo aliyemfanya mtu ashindwe kuzungumza. Ikawa, pepo alipotoka, yule mtu akaanza kuongea, umati wa watu walishangaa. 15 Lakini baadhi ya watu walisema, “Anatumia nguvu za Shetani kuwatoa pepo. Shetani[a] ni mtawala wa pepo wachafu.”

16 Baadhi ya watu wengine waliokuwa pale walitaka kumjaribu Yesu, walimwomba afanye muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. 17 Lakini alijua walichokuwa wanafikiria, hivyo akawaambia, “Kila ufalme unaopigana wenyewe huteketezwa; na familia yenye magomvi husambaratika. 18 Hivyo, ikiwa Shetani anapigana yeye mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Ninawauliza hivi kwa kuwa mnasema kwamba ninatoa pepo kwa kutumia nguvu za Shetani. 19 Lakini ikiwa ninatoa pepo kwa kutumia nguvu za Shetani, watu wenu wanatumia nguvu gani wanapotoa pepo? Hivyo watu wenu wenyewe watathibitisha kuwa ninyi ni waovu. 20 Lakini, ninatumia nguvu za Mungu kutoa pepo. Hii inaonesha kuwa Ufalme wa Mungu umekuja kwenu sasa.

21 Mwenye nguvu aliye na silaha nyingi anapoilinda nyumba yake, vitu vilivyomo ndani ya nyumba yake huwa salama. 22 Lakini chukulia kuwa mwenye nguvu zaidi kuliko yeye akimshambulia na kumshinda, yule mwenye nguvu zaidi humnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea kuilinda nyumba yake. Ndipo mwenye nguvu zaidi atavitumia vitu vya yule mtu wa kwanza kadri anavyotaka.

23 Mtu yeyote asiye pamoja nami, yuko kinyume nami. Na mtu yeyote asiyefanya kazi pamoja nami anafanya kinyume nami.

Hatari ya Kuwa Mtupu

(Mt 12:43-45)

24 Mtu anapotokwa na roho chafu, roho hiyo husafiri sehemu zilizo kavu, ikitafuta mahali ili ipumzike. Lakini hukosa mahali pa kupumzika. Hivyo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba nilikotoka.’ 25 Inaporudi hukuta nyumba imesafishwa na kupangwa vizuri. 26 Ndipo roho hiyo chafu huenda ikachukua roho wengine saba, walio waovu kuliko yenyewe. Na kwa pamoja roho zote hizo huingia na kuishi ndani ya mtu huyo, na mtu huyo hupata matatizo mengi kuliko ya kwanza.”

Watu Wanaobarikiwa na Mungu

27 Yesu alipokuwa akisema mambo haya, mwanamke mmoja katika kundi la watu akapaza sauti akamwambia “Amebarikiwa na Mungu mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!”

28 Lakini Yesu akasema, “Wamebarikiwa zaidi wanaosikia na kuyatii mafundisho ya Mungu.”

Baadhi ya Watu Wawa na Mashaka na Mamlaka ya Yesu

(Mt 12:38-42; Mk 8:12)

29 Baada ya kundi la watu kuongezeka na kumzunguka, Yesu alisema, “Ninyi watu mnaoishi sasa ni waovu. Mnaomba muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika ili kuwathibitishia jambo lolote. Ishara pekee mtakayopata ni kile kilichompata Yona.[b] 30 Yona alikuwa ishara kwa watu walioishi katika mji wa Ninawi. Ni sawasawa na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa watu wa wakati huu.

31 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa, mtalinganishwa na Malkia wa Kusini,[c] naye pia, atakuwa shahidi atakayeonyesha namna mlivyo waovu. Kwa nini ninasema haya? Kwa sababu alisafiri kutoka mbali, mbali sana ili ayasikilize mafundisho yenye hekima ya Suleimani. Na ninawaambia mkuu[d] kuliko Suleimani yupo hapa, lakini hamnisikilizi!

32 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa mtafananishwa pia na watu wa Ninawi, nao watakuwa mashahidi watakaoonyesha makosa yenu. Ninasema hivi kwa sababu Yona alipowahubiri, walibadili mioyo na maisha yao. Na sasa mnamsikia mtu aliye mkuu kuliko Yona, Lakini hamtaki kubadilika!

Iweni Mwanga kwa Ajili ya Ulimwengu

(Mt 5:15; 6:22-23)

33 Hakuna mtu anayechukua taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunika. Badala yake huiweka mahali palipo wazi, ili wanaoingia ndani waweze kuiona nuru yake. 34 Namna unavyowatazama watu inaonesha kwa hakika jinsi ulivyo. Unapowatazama watu katika hali isiyo ya ubinafsi, inaonesha wazi kuwa umejaa nuru. Lakini unapowatazama watu katika namna ya uchoyo, ni wazi kuwa umejaa giza.[e] 35 Hivyo iweni waangalifu ili nuru iliyo ndani yenu usiwe giza! 36 Ikiwa umejaa nuru na hakuna sehemu yenye giza ndani yako, basi utang'aa, kama nuru ya kwenye taa.”

Yesu Awakosoa Viongozi wa Kidini

(Mt 23:1-36; Mk 12:38-40; Lk 20:45-47)

37 Baada ya Yesu kumaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika Yesu kula pamoja naye. Hivyo Yesu alikwenda na kuketi sehemu ya kulia chakula. 38 Lakini Farisayo alishangaa alipoona Yesu hakunawa[f] mikono yake kwanza kabla ya kuanza kula. 39 Bwana akamwambia, “Usafi mnaoufanya ninyi Mafarisayo ni kama kusafisha kikombe au sahani kwa nje tu. Lakini ndani yenu mna nini? Mnataka kuwadanganya na kuwaumiza watu tu. 40 Ninyi ni wajinga! Aliyeumba kilicho nje ndiye aliumba kilicho ndani. 41 Hivyo, jalini vilivyo ndani. Wapeni vitu wenye uhitaji. Ndipo mtakuwa wasafi kikamilifu.

42 Lakini, ole wenu ninyi Mafarisayo! Mnampa Mungu sehemu ya kumi ya vyakula mnavyopata, hata mnanaa, na hata kila mmea mdogo katika bustani[g] zenu. Lakini mnapuuzia kuwatendea haki wengine na kumpenda Mungu. Haya ni mambo mnayotakiwa kufanya. Na endeleeni kufanya mambo hayo mengine.

43 Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kupata viti vya heshima katika masinagogi. Na mnapenda kusalimiwa na watu kwa kuheshimiwa sehemu za masoko. 44 Ole wenu, kwa kuwa mnafanana na makaburi ya zamani yasiyoonekana, ambayo watu hupita juu yake na kuyakanyaga bila kuyatambua.”

45 Mmoja wa wanasheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, unaposema mambo haya kuhusu Mafarisayo unatukosoa hata sisi pia.”

46 Yesu akamjibu, “Ole wenu, enyi wanasheria! Mnatunga sheria kali ambazo ni vigumu watu kuzitii.[h] Mnawalazimisha wengine kuzitii sheria zenu. Lakini ninyi wenyewe hamthubutu hata kujaribu kufuata mojawapo ya sheria hizo. 47 Ole wenu kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii. Lakini hawa ni manabii wale wale ambao mababu zenu waliwaua. 48 Na sasa mnawaonesha watu wote kwamba mnakubaliana na mambo ambayo baba zenu walifanya. Waliwaua manabii, nanyi mnasherehekea mauaji hayo kwa kujenga makaburi ya manabii! 49 Hii ndiyo sababu ambayo kwa Hekima yake Mungu alisema, ‘Nitawatuma manabii na mitume[i] kwao. Baadhi ya manabii na mitume wangu watauawa na watu waovu. Wengine watateswa sana.’

50 Hivyo ninyi watu mnaoishi sasa mtaadhibiwa kwa sababu ya vifo vya manabii wote waliouawa tangu mwanzo wa ulimwengu. 51 Mtachukuliwa wenye hatia kutokana na vifo hivyo vyote, tangu kuuawa kwa Habili mpaka kuuawa kwa nabii Zakaria,[j] aliyeuawa kati ya madhabahu na Hekalu. Ndiyo ninawaambia, kizazi hiki kitaadhibiwa kwa sababu yao wote.

52 Ole wenu, ninyi wanasheria, mmechukua ufunguo wa kujifunza kuhusu Mungu. Ninyi wenyewe hamtaki kujifunza na mmewazuia wengine wasijifunze pia.”

53 Yesu alipotoka humo, walimu wa sheria na Mafarisayo walianza kumpinga sana. Walianza kumjaribu ili awajibu maswali kuhusu mambo mengi, 54 ili Yesu akisema jambo isivyo sahihi waweze kupata sababu ya kumkosoa.

Footnotes

  1. 11:15 Shetani Jina la Mwovu lenye maana “Adui”. Kwa maana ya kawaida, “Beelzebuli” kwa Kiyunani (mwovu). Pia katika mstari wa 18,19.
  2. 11:29 Yona Nabii katika Agano la Kale. Baada ya siku tatu akiwa katika tumbo la samaki, alitoka akiwa hai. Kisha alikwenda katika mji uliojaa uovu, mji wa Ninawi ili kuwapa watu maonyo ya Mungu.
  3. 11:31 Malkia wa Kusini Au “Malkia wa Sheba.” Alisafiri kama maili 1,000 (kilomita 1,600) ili kujifunza hekima ya Mungu kutoka kwa Sulemani. Tazama 1 Fal 10:1-13.
  4. 11:31 mkuu Kwa maana ya kawaida, “mtu mkuu zaidi”. Pia katika mstari wa 32.
  5. 11:34 Kwa maana ya kawaida, “Taa ya mwili ni jicho lako. Unapowatazama watu bila kuwa na kinyongo, mwili wako wote unakuwa umejaa nuru. Lakini ikiwa jicho lako ni la uovu, mwili wako una giza.”
  6. 11:38 hakunawa Hakunawa kwa maana ya kuwa kunawa mikono au kuoga mwili wote ilikuwa desturi ya dini ya Kiyahudi na Mafarisayo waliipa desturi hii umuhimu mkubwa.
  7. 11:42 Mnampa … bustani Kwa maana ya kawaida, “Mnatoa zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga mboga.” Sheria ya Musa iliwataka Waisraeli kushirikiana chakula kwa kutenga sehemu ya kumi ya mazao na mifugo yao kwa ajili ya Mungu (tazama Law 27:30-32; Kum 26:12). Hii haikujumuisha mazao madogo ya bustani kama yaliyotajwa hapa. Hivyo Mafarisayo hawa walikuwa wanatoa zaidi ya inavyotakiwa ili kuhakikisha kuwa hawavunji sheria.
  8. 11:46 Mnatunga sheria kali … watu kuzitii Kwa maana ya kawaida, “Mnawatwisha watu mizigo wasiyoweza kuibeba.”
  9. 11:49 manabii na mitume Watu waliochaguliwa na Mungu kuhubiri Habari Njema ulimwenguni.
  10. 11:51 Habili … Zakaria Katika Agano la Kale la Kiebrania, hawa ni watu wa kwanza na wa mwisho kuuawa. Tazama Mwa 4:8-11 na 2 Nya 24:20-25.