Wagalatia 3:26-4:7
Neno: Bibilia Takatifu
26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na
Wana Wa Mungu
4 Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Copyright © 1989 by Biblica