Wasaidieni Wakristo Wenzenu

Hakuna sababu ya kuwaandikia kuhusu msaada unaotolewa kwa ajili ya watu wa Mungu, kwa kuwa ninajua mlivyo tayari kutoa, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili yenu kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Ari yenu imewachochea wengi wao kuanza kutoa. Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusije kukawa ni maneno matupu, bali muwe tayari kama nilivyosema mko tayari. Isije ikawa nitakapokuja na watu wa Makedonia nikute hamko tayari niaibike, na ninyi zaidi, kwa kuwa nilishasema mko tayari. Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kabla yangu, wafanye mipango yote ya matoleo ya zawadi mliyoahidi ili iwe tayari, si kama mchango wa kulazim ishwa bali kama zawadi ya hiari.

Kumbukeni kwamba, mtu anayepanda mbegu chache, atavuna mazao machache; na mtu anayepanda mbegu nyingi atavuna mazao mengi. Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa kusita au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu anapenda mtu anayetoa kwa moyo. Na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kila kazi njema. Kama Maandiko yanavyosema, “Yeye hutapanya kila mahali kuwapa maskini, haki yake hudumu milele.” 10 Na Mungu ambaye ndiye humpa mkulima mbegu za kupanda, na mkate kwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu mnazohitaji na kuziwezesha kukua zitoe mazao ya matendo mema ya haki. 11 Atawa fanya kuwa matajiri kwa kila hali ili mpate kuwa wakarimu kila wakati na kwa mchango wenu wa hiari kupitia kwetu, wengi wapate kumshukuru Mungu. 12 Huduma hii mnayofanya si kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu, bali utaleta mbubujiko wa shukrani nyingi kwa Mungu tu. 13 Kwa kutoa kwenu, mtakuwa mnatoa uthibitisho wa uhakika wa imani yenu. Ndipo watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu unaoambatana na kukiri kwenu kwa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wa mchango wenu kwao na kwa wen gine wote. 14 Nao watawaombea kwa upendo mwingi kwa ajili ya neema kuu mliyopewa na Mungu. 15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi hii isiyoelezeka.