Hazina Za Roho Kwenye Vyombo Vya Udongo

Kwa hiyo tukiwa na huduma hii kwa rehema ya Mungu, hatu kati tamaa. Tumekataa njia za siri na za aibu. Hatutumii njia za udanganyifu, wala hatupotoshi neno la Mungu. Badala yake, tunaeleza neno la kweli wazi wazi na kujitambulisha kuwa wa kweli kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu. Na hata kama Injili yetu imefichika, basi imefichika kwa wale wanaopotea. Kwa upande wao, mungu wa dunia hii ametia giza akili za wasioamini, ili wasione mwanga wa Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ana sura ya Mungu. Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung’aao katika uso wa Kristo.

Hata hivyo tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kuonyesha kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, na si kutoka kwetu. Tumegandamizwa kila upande, lakini hatujashindwa. Tumetatanishwa lakini hatukati tamaa; tumeteswa lakini hatuku achwa upweke; tumetupwa chini lakini hatujateketezwa. 10 Tuna chukua katika mwili wetu kifo cha Yesu wakati wote ili uhai wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 11 Kwa maana sisi tunaoishi, maisha yetu yako katika hatari ya kifo wakati wote kwa ajili ya Yesu ili uhai wake uweze kuonekana katika miili yetu ya mauti. 12 Kwa hiyo, mauti inatuandama wakati wote, bali uzima unafanya kazi ndani yenu. 13 Maandiko yanasema, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Sisi pia tunaamini, kwa hiyo tunasema. 14 Kwa maana tunajua ya kuwa aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu na kutufikisha sisi na ninyi mbele zake. 15 Haya yote ni kwa ajili yenu, ili kwa kadiri neema ya Mungu inavyowafi kia watu wengi zaidi, wote watoe shukrani kwa utukufu wa Mungu.

16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa miili yetu inachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya kila siku. 17 Maana hii dhiki yetu nyepesi na ya muda mfupi inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa uzima wa milele unaozidi sana matatizo haya. 18 Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.