Paulo Na Mitume Wa Uongo

11 Natumaini mtanivumilia hata wakati ninapokuwa mjinga kidogo. Tafadhali nivumilieni! Nawaonea wivu wa kimungu kwa kuwa mimi niliwaposea Kristo, ili niwatoe kama mwanamwali anavy otolewa kwa mume mmoja akiwa hana dosari. Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa na ujanja wa yule nyoka, huenda akili zenu zimepotoshwa, mkaacha upendo wenu safi na wa kweli kwa Kristo. Kwa sababu kama mtu akija akawahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au kama mkikubali Injili nyingine ambayo si ile mliyoikubali, mnaipokea kwa moyo mmoja! Lakini sidhani ya kuwa mimi ni mdogo sana nikilinganishwa na hao ‘mitume wakuu’. Hata kama mimi si mzungumzaji hodari, lakini ni hodari katika maarifa. Jambo hili ni dhahiri kwenu.

Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha mbele yenu na kuwainua ninyi, kwa kuwa niliwahubiria Injili ya Mungu pasipo gharama yo yote kwa upande wenu? Nilipokea msaada kutoka kwa makanisa men gine, niliwanyang’anya wao ili niweze kuwahudumia ninyi. Na nilipokuwa nanyi, nikipungukiwa na cho chote, sikuwa mzigo kwa mtu ye yote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walitosheleza mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia na nitaendelea kujizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yo yote. 10 Na kama ukweli wa Kristo ulivyo ndani yangu, hakuna mtu ye yote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. 11 Kwa nini? Mnadhani ni kwa kuwa siwa pendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda!

12 Nami nitaendelea kufanya hivi ili kuwazima wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia. 13 Watu kama hao ni manabii wa uongo, ni wafany akazi wadanganyifu ambao wanajifanya kuwa mitume wa Kristo. 14 Na hii si ajabu, kwa sababu hata shetani hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 15 Kwa hiyo si ajabu kama malaika wake shetani nao wanajigeuza waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao.

Paulo Anajivunia Mateso Yake

16 Nasema tena, mtu ye yote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 17 Ninayosema sasa, kwa majivuno, nasema kama mjinga na wala si kwa mamlaka ya Bwana. 18 Kwa sababu wengine wanajivunia mambo ya kidunia, basi na mimi nitaji sifu. 19 Ninyi mnawavumilia wajinga kwa kuwa mna hekima mno! 20 Tena mnavumilia hata kama mtu anawafanya watumwa au anawany onya na kuwadanganya au anajigamba mbele yenu au anawapiga makofi usoni. 21 Naona aibu kukubali kwamba sisi ni wadhaifu kiasi ambacho hatuwezi kufanya mambo kama hayo. Lakini cho chote ambacho mtu anathubutu kujivunia, sasa nasema kama mjinga, mimi pia naweza kuthubutu kujivunia.

22 Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 23 Wao ni watumishi wa Kristo? Mimi ni mtumishi bora zaidi, nasema kama kichaa. Nimefanya kazi zaidi, nimefungwa gerezani zaidi, nimechapwa viboko visivyo na hesabu, na mara nyingi nilikuwa karibu kufa. 24 Mara tano nimechapwa viboko aro baini kupungua kimoja na Wayahudi. 25 Nimechapwa kwa chuma mara tatu. Nimepigwa mawe mara moja. Mara tatu nimevunjikiwa na meli. Nimeelea baharini usiku kucha na mchana kutwa. 26 Katika safari zangu nyingi, nimekuwa katika hatari za mafuriko, hatari za wany ang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu na hatari kutoka kwa watu wa mataifa mengine; nimekuwa katika hatari mijini, nyikani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 27 Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, siku nyingi nimekuwa bila usingizi, nimekuwa na njaa na kiu, mara nyingi nimekuwa bila chakula, katika baridi na bila nguo. 28 Na ukiacha mambo mengine nimelemewa na wasiwasi juu ya makanisa yote. 29 Je, ni nani ana kuwa mdhaifu nisijisikie mdhaifu? Nani anashawishiwa kutenda dhambi nisijisikie nachomwa na uchungu?

30 Nikilazimika kujisifu, basi nitajisifia yale mambo yanay oonyesha udhaifu wangu. 31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye amebarikiwa daima, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 32 Kule Dameski, gavana aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliu linda mji wa Dameski ili wapate kunikamata, 33 lakini nilish ushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani nikaepuka kukamatwa.