Kutoka kwa Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu. Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Ninakutakia neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Paulo Amtia Moyo Timotheo

Ninamshukuru Mungu ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyomtumikia baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika sala zangu. Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nijazwe furaha. Nakumbushwa kuhusu imani yako ya kweli, imani ambayo walikuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo nina hakika, unayo. Kwa sababu hii nakukum busha ukichochee kile kipawa ulichopewa na Mungu wakati nilipo kuwekea mikono. Maana Mungu hakutupatia roho ya woga bali roho ya nguvu, ujasiri na kiasi.

Basi usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake, bali uishiriki taabu kwa ajili ya Habari Njema kwa kadiri ya nguvu upewayo na Mungu. Yeye ametuokoa na kutuita tupokee maisha ya utakatifu; si kwa sababu ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya makusudio yake na neema yake. Tulipewa neema hii katika Kristo Yesu tangu milele 10 na sasa imedhihirishwa kwa kuja kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu ambaye ameondoa kifo kabisa na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11 Nami nimechaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 12 Ndio sababu ninateseka hivi. Lakini sioni aibu kwa maana ninamjua huyo niliyemwamini na nina hakika ya kuwa anaweza kutunza kile nilichomkabidhi, mpaka siku ile.

13 Tumia kama kielelezo cha mafundisho sahihi maneno ya kweli ambayo umeyasikia kutoka kwangu pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 14 Linda ile kweli ambayo umekabidhiwa na Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu. 15 Bila shaka unafahamu kuwa watu wote katika jimbo la Asia wameniacha, wakiwemo Filego na Hermogene. 16 Bwana aonyeshe huruma yake kwa jamaa ya Onesiforo kwa sababu alinitia moyo mara nyingi na hakuonea aibu minyororo yangu. 17 Bali alipofika Roma alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana amwezeshe kupata rehema kutoka kwa Bwana siku ile. Unafahamu pia jinsi alivyoni saidia huko Efeso.

Salamu kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu.[a] Ni mtume kwa sababu ndivyo Mungu alivyotaka. Yeye alinituma kwa sababu Mungu alipenda niwaeleze watu juu ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu.

Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:

Neema, rehema na amani iwe kwako kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.

Shukrani na Kutia Moyo

Daima namshukuru Mungu katika maombi yangu ninapokukumbuka usiku na mchana kwa ajili yako. Ni Mungu wa mababu zangu na daima nimemtumikia kwa dhamiri safi. Nikiyakumbuka machozi yako kwa ajili yangu, ninatamani kukuona, ili niweze kujazwa na furaha. Nimekumbuka imani yako ya kweli ambayo mwanzoni ilikuwa kwa bibi yako Loisi na kwa mama yako Eunike. Nami nashawishika hiyo iko kwako. Kwa sababu hii ninakukumbusha karama ya Mungu ambayo uliipokea wakati nilipokuwekea mikono. Sasa nataka uitumie karama hiyo na ikue zaidi na zaidi kama mwali wa moto mdogo uwakavyo ndani ya moto. Kwani Roho ambaye Mungu alitupa sisi ni chanzo cha ujasiri wetu, ni nguvu, upendo na fikra safi.

Hivyo usione aibu kushuhudia juu ya Bwana wetu Yesu au kunionea aibu mimi, niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali aliteseka pamoja nami kwa ajili ya Habari Njema na Mungu hutupa nguvu.

Alituokoa na kutuita katika maisha ya utakatifu, sio kwa sababu ya kitu cho chote tulichokifanya wenyewe, bali kwa kusudi lake mwenyewe na neema, ambayo ametupa sisi kwa Kristo Yesu kabla ya mwanzo wa wakati, 10 na ambayo sasa imeonyeshwa kwetu kwa kuja kwake Kristo Yesu, Mwokozi wetu. Yeye Kristo aliiharibu mauti na kuleta uzima na kutokufa kwenye nuru kwa njia ya Habari Njema.

11 Niliteuliwa na Mungu kutangaza Habari Njema kama mtume na mwalimu. 12 Na ni kwa kazi hii ninateseka lakini sioni haya kwa sababu namjua yeye niliyemwekea imani yangu, na nina uhakika kuwa anaweza kukilinda kile nilichokikabidhi kwake hadi Siku ile.

13 Yale uliyoyasikia nikiyafundisha yawe mfano kwako wa mafundisho utakayofundisha wewe. Uyafuate na yawe kielelezo cha mafundisho ya kweli na uzima kwa uaminifu na upendo ule ule ambao Kristo Yesu ametuonesha. 14 Kwa msaada wa Roho Mtakatifu anayeishi ndani yako, uyalinde mafundisho haya ya mazuri na yenye thamani mliyopewa dhamana kwayo.

15 Unajua kwamba kila mtu aliyeko Asia ameniacha. Hata Figelo na Hermogene nao wameniacha. 16 Ninaomba kwamba Bwana ataonesha rehema wa familia ya Onesiforo, amekuwa faraja yangu mara nyingi, na hakuona haya kwa ajili yangu kuwa gerezani. 17 Kinyume chake, alipofika Rumi, alinitafuta kwa bidii hadi aliponiona. 18 Bwana Yesu na amjalie kupata rehema kutoka kwa Bwana Mungu katika siku ile ya hukumu ya mwisho! Unafahamu vema ni kwa njia ngapi alinihudumia wakati nilipokuwa Efeso.

Footnotes

  1. 1:1 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.