Imani Ndani Ya Kristo

Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo, ni mtoto wa Mungu; na kila ampendaye mzazi wa mtoto, humpenda pia na mtoto wa mzazi huyo. Na hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: tukimpenda Mungu na kuzitii amri zake. Kwa maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri zake hazitule mei. Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu ameushinda ulimwengu. Nasi tumeushinda ulimwengu kwa imani yetu. Ni nani basi aushin daye ulimwengu isipokuwa yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Mashahidi Wa Yesu Kristo

Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na damu; si kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Roho mwenyewe ndiye anayemshu hudia kwa maana Roho ni kweli. Wapo mashahidi watatu: Roho, maji na damu; na hawa watatu wanakubaliana. Kama tunakubali ushahidi wa wanadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; kwa sababu huu ni ushahidi wa Mungu ambao ameutoa kumhusu Mwanae. 10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.

Uzima Wa Milele

13 Ninawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu kusudi mjue kuwa mnao uzima wa milele. 14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia. 15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.

Umuhimu Wa Kuonyana

16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.

18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa. 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na kwamba ulim wengu wote unatawaliwa na yule mwovu. 20 Tunajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa ufahamu ili tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.