Matoleo Kwa Ajili Ya Waamini

16 Na sasa kuhusu matoleo kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Mungu. Kama nilivyoagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake, na fedha hiyo aiweke ili nitaka pokuja pasiwepo na haja ya kufanya mchango. Nikishafika nita wapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili waweze kupeleka zawadi yenu Yerusalemu. Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.

Mipango Ya Paulo

Baada ya kupitia Makedonia, nitakuja kwenu; maana natazamia kupitia Makedonia. Pengine nitakaa nanyi kwa muda, au hata nitakaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili muweze kunisaidia katika safari zangu, po pote niendapo. Kwa maana sipendi niwaone sasa nikiwa napita; natarajia kuwa na muda wa kutosha wa kukaa nanyi, kama Bwana akiruhusu. Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste. Kwa maana mlango umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, na huko kuna wapinzani wengi . 10 Ikiwa Timotheo atakuja kwenu mkaribisheni asiwe na woga wo wote akiwa nanyi kwa sababu anaendeleza kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo. 11 Basi asiwepo mtu atakayemdharau. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunirudia. Namtegemea yeye pamoja na hao ndugu.

12 Na sasa, kuhusu ndugu yetu Apolo. Nilimsihi sana awa tembelee pamoja na wale ndugu wengine, lakini haikuwa mapenzi yake kuja huko wakati huu. Atakuja apatapo nafasi.

Maneno Ya Mwisho

13 Kesheni; simameni imara katika imani, muwe shujaa na hodari. 14 Fanyeni kila kitu katika upendo. 15 Sasa ndugu zangu, mnafahamu kwamba watu wa nyumbani kwa Stefana walikuwa waamini wa kwanza katika Akaya, nao wamejitoa kuwasaidia watu wa Mungu. 16 Nawasihi mnyenyekee na kufuata uongozi wa watu kama hawa, na wa kila mtendakazi mwenzenu na kila anayejibidisha katika kazi. 17 Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa maana hawa wamenisaidia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. 18 Wao wameburudisha roho yangu na yenu pia. Watu kama hawa, wanastahili kutambuliwa. 19 Makanisa ya Asia wanawas alimu. Akila na Priska, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu katika Bwana. 20 Pia ndugu wote wanawasalimu. Sali mianeni kwa busu takatifu. 21 Mimi Paulo, kwa mkono wangu mwe nyewe, naandika salamu hii. 22 Kama mtu ye yote hampendi Bwana, na alaaniwe. ‘Maranatha.’ Bwana wetu, njoo! 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.