Kutoka kwa Paulo, aliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo, na Sosthene ndugu yetu.

Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wote waliota kaswa katika Kristo Yesu, wakaitwa wawe watakatifu, pamoja na wengine wote ambao kila mahali wanalikiri jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wao na Bwana wetu. Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

Baraka Zitokazo Kwa Kristo

Ninamshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema aliyowapa ndani ya Kristo Yesu. Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kunena kwenu, katika maarifa yote, kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.

Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa

10 Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane ninyi kwa ninyi, na pasiwepo na utengano kati yenu. Muungane pamoja kikamilifu katika kuwaza na katika kuamua. 11 Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa watu wa nyumbani kwa Kloe kwamba kuna ugomvi kati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: mmoja wenu anasema, “Mimi ni wa Paulo,” mwin gine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”

13 Je, Kristo amegawanyika? Je, ni Paulo aliyewafia msala bani? Au mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwa sababu sikumbatiza mtu ye yote isipokuwa Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyo hakuna mtu kati yenu anayeweza kusema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 Ndiyo nakumbuka, pia niliwabatiza Stefano na watu wa nyumbani kwake. Lakini zaidi ya hao sikumbuki kama nilimbatiza mtu mwingine. 17 Kwa maana Kristo hakunituma kubatiza bali kuhu biri Injili na nifanye hivyo pasipo kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu, ili nguvu ya kifo cha Kristo msalabani iwe dhahiri.

Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu

18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Maan diko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.” 20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22 Way ahudi wanataka ishara, Wagiriki wanatafuta hekima. 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa msalabani, ujumbe ambao ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa Wagiriki ni upuuzi. 24 Lakini kwa walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25 Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.

26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa Mungu alipowaita. Si wengi mlikuwa na hekima kwa kipimo cha kibinadamu. Si wengi mli kuwa na vyeo na si wengi mlikuwa wa jamaa za kifahari. 27 Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu alichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa humu duniani, vitu ambavyo si kitu, ili avibatilishe vile ambavyo vinaonekana kuwa vya maana; 29 ili mtu ye yote asijisifu mbele yake. 30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi 31 Kwa hiyo, kama Maan diko yasemavyo: “Mtu ye yote anayetaka kujisifu, basi ajisifu kwa ajili ya Bwana.”